Vikwazo dhidi ya Iran kurejeshwa kutokana na shughuli za nyuklia zilizopigwa marufuku

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vikwazo vikubwa vya kiuchumi na kijeshi dhidi ya Iran vilivyoondolewa chini ya makubaliano ya kihistoria ya kimataifa kuhusu mpango wake wa nyuklia miaka 10 iliyopita vinatarajiwa kurejeshwa Jumamosi

Vikwazo vilidhoofisha uchumi wa Iran kabla ya kuondolewa chini ya makubaliano ya 2015

Haya yanajiri baada ya Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kuliandikia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi uliopita, na kuishutumu Iran kwa kushindwa kutekeleza ahadi zake. Hilo lilizua utaratibu wa kuipa Iran siku 30 kutafuta suluhu la kidiplomasia ili kuepusha vikwazo vilivyowekwa upya.

Iran imeitaja hatua hiyo kuwa kinyume cha sheria na inasema kuwa itasimamisha ushirikiano na shirika la kimataifa la nyuklia la Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) iwapo vikwazo vitarejeshwa.

Iran ilizidisha shughuli iliyopigwa marufuku ya nyuklia baada ya Marekani kujiondoa katika makubaliano hayo mwaka 2016.

Wapalestina 40 wauawa katika Ukanda wa Gaza

Operesheni ya kijeshi ya Israeli huko Gaza, Septemba 26, 2025

Wapalestina 40 wameuawa katika eneo lote la Ukanda wa Gaza tangu alfajiri ya Jumamosi, “huku mashambulizi makali ya anga na ubomoaji wa nyumba yakiendelea” na vikosi vya Israel, kwa mujibu wa shirika la habari la Palestina WAFA.

Duru za kitabibu ziliiambia WAFA kuwa “mashahidi 40 wameuawa katika Ukanda wa Gaza tangu alfajiri ya leo.

Mashahidi tisa walifika katika Hospitali ya Al-Shifa, 14 katika Hospitali ya Al-Ahli Arab Baptist, 10 katika Hospitali ya Al-Awda, mmoja katika Hospitali ya Nasser, na sita katika Hospitali ya Al-Aqsa.”

Alibainisha kuwa “miongoni mwa mashahidi, kulikuwa na shahidi aliyekuwa akitafuta msaada katika eneo la Netzarim.”

Rais wa Marekani Donald Trump alisema Ijumaa kuwa mazungumzo kuhusu Gaza na nchi za Mashariki ya Kati yalikuwa ya kina.

Ameongeza kuwa Israel na Hamas wanafahamu kuhusu mazungumzo hayo, na kusema kuwa mazungumzo hayo yataendelea kadiri inavyohitajika ili kufikia makubaliano.

Trump alikutana na viongozi na maafisa kutoka nchi kadhaa zenye Waislamu wengi wiki hii kujadili hali ya Gaza, ambayo inashambuliwa na mshirika wa Washington, Israel.

Mjumbe Maalumu wa Marekani Steve Witkoff alisema kuwa Trump aliwasilisha mapendekezo kwa viongozi hao, ikiwa ni pamoja na mpango wa amani wa Mashariki ya Kati wenye vipengee 21.

Watu 100 wahofiwa kupoteza maisha kwa kufukiwa mgodini Nigeria

Takribani watu 100 wanahofiwa kufariki dunia baada ya kufukiwa na vifusi vya mgodi wa dhahabu katika jimbo la Zamfara, kaskazini magharibi mwa Nigeria.

Mgodi huo uliopo katika eneo la Kadauri, wilaya ya Maru, uliporomoka Alhamisi wakati wachimbaji wa kawaida wakifanya kazi chini ya ardhi, kwa mujibu wa Reuters.

Operesheni za uokoaji ziliendelea hadi Ijumaa. Sanusi Auwal, mkazi wa eneo hilo aliyehusika katika juhudi za uokoaji, alisema kwamba miili 13 tayari imetolewa kutoka kwenye mabaki ya mgodi, ikiwa ni pamoja na mwili wa binamu yake.

“Zaidi ya wachimbaji 100 walikuwepo chini wakati mgodi ulipoporomoka,” Auwal alisema kwa simu. “Tuna bahati tumeokolewa hai. Tulikuwa zaidi ya watu 100, sisi 15 tu ndio tuliookolewa,” alisema Isa Sani, ambaye kwa sasa anapatiwa matibabu kutokana na majeraha.

Muhammadu Isa wa chama cha wachimbaji wa jimbo la Zamfara alithibitisha tukio hilo, akiongeza kwamba baadhi ya waokoaji walipata Dhoruba wakati wakijaribu kutoa waathirika.

Msemaji wa polisi wa Zamfara, Yazid Abubakar, hakutoa maelezo alipoombwa kwa simu na ujumbe wa maandishi kutoa maoni yake. Uchimbaji haramu ni wa kawaida Zamfara, ambapo makundi yenye silaha mara nyingi hushikilia uongozi wa migodi ya dhahabu, hali inayochochea vurugu na ajali zinazosababisha vifo.

Kiongozi wa biashara ya ngono Dubai akamatwa baada ya uchunguzi wa BBC

Mwezigwa

Kiongozi wa mtandao wa biashara ya unyanyasaji wa ngodo kwa wanawake wenye uwezo mdogo, ambao uliwatumia wanawake kufanya kazi katika miji ya kifahari zaidi ya Dubai, amekamatwa nchini Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), BBC imeripoti.

Charles Abe Mwezigwa, aliyetambuliwa kama mkurugenzi wa mtandao huo katika uchunguzi wa hivi karibuni wa BBC, alikamatwa baada ya kufanya mikutano ya siri na mwandishi wa BBC aliyejifanya mteja.

Katika video hizo, Mwezigwa alisema angeweza kumpa mtu aliyehitaji mwanamke kwa ajili ya ngono kwa kiasi cha dola 1,000 tu.

Mkurugenzi huyo pia alisema wanawake wake “wanaweza kufanya karibu chochote kinachotakiwa na wateja,” na akafichua kuwa kabla ya hili alifanya kazi kama dereva wa basi huko London.

Kampuni ya sheria ya Dubai ilithibitisha kuwa Mwezigwa anashikiliwa katika Gereza kuu la Al Awir, Dubai, huku Interpol ikitoa tangazo la kumtafuta kimataifa.

Uchunguzi wa BBC ulijumuisha ushuhuda wa mabinti wadogo wa Uganda waliopelekwa Dubai kwa ahadi za ajira, lakini badala yake walilazimishwa kushiriki katika biashara ya ngono.

Baadhi walisema walidhani watakuwa wakifanya kazi katika sehemu za kawaida kama vile maduka makubwa au hoteli.

Masuala ya ngono ni kinyume cha sheria huko Dubai. Mmoja wa wahusika, aliyejulikana kama “Mia” sio jina lake halisi wa ajili ya kumlinda, alieleza kuwa aliangukia kwenye mtego wa Mwezigwa, na kwamba angalau mteja mmoja aliomba mara kwa mara kufanya vitendo vya unyama.

Mwezigwa amekanusha madai yote yaliyotolewa na uchunguzi wa BBC, akisema kuwa anasaidia wanawake kupata makazi kama ‘dalali’ kati ya wanawake hao na wenye nyumba, na kwamba wanawake huenda kwenye sherehe naye kutokana na yeye kuwa na ukaribu na na matajiri” wa Dubai. Aliongeza: “Nimesema kuwa mimi ni mtu wa sherehe tu.

Ninawaalika watu wanaotumia kwa ukarimu mezani kwangu, jambo linalovutia wasichana wengi kunifuata. Hivyo ninajua wasichana wengi, ni hicho tu.”

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment