Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa Marekani amesema hayo kabla ya hotuba ya Waziri Mkuu wa Israel katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza ushuru mpya kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje, ikiwemo dawa na malori.
Ametangaza kuongeza ushuru hadi asilimia 100 kwa dawa zinazotengenezwa nje kwa kutumia leseni za kampuni za Kimarekani, au zile zinazozalishwa ndani ya Marekani lakini kuuzwa kwa majina tofauti.
Hatua hii itaanza kutekelezwa kuanzia Oktoba 1, isipokuwa kwa kampuni zitakazojenga viwanda vya uzalishaji ndani ya Marekani.
Aidha, serikali ya Marekani imeweka ushuru wa asilimia 25 kwa malori makubwa ya kubeba mizigo, huku ushuru kwa vifaa vya jikoni na vya bafuni ukiongezwa kwa asilimia 50.
Rais Trump amesema kuwa hatua hiyo inalenga kulinda masoko ya ndani.
“Bidhaa nyingi kutoka nje zinaingizwa kwa bei ya kutupwa nchini mwetu, hali ambayo imeyasukuma bidhaa za ndani nje ya soko,” alisema kupitia ukurasa wake wa Truth Social.
Hata hivyo, hatua hiyo imezua pingamizi kutoka kwa wafanyabiashara wa Marekani, ambao wametoa wito kwa Ikulu ya White House kusitisha ushuru huo wa ziada.
Israel yashambulia ngome za Wahouthi mjini Sanaa, yaua na kujeruhi kadhaa

Israel imetekeleza mashambulizi dhidi ya mji mkuu wa Yemen, Sanaa, siku ya Alhamisi, kwa mujibu wa vyombo vya habari vinavyohusiana na Wahouthi pamoja na Waziri wa Ulinzi wa Israel.
Mashambulizi hayo yamesababisha vifo na majeruhi kadhaa.
Mashambulizi hayo yanakuja siku moja baada ya watu kadhaa kujeruhiwa katika mji wa Eilat, Israel, siku ya Jumatano, kufuatia shambulizi la ndege zisizo tumia rubani lililodaiwa na kundi la Wahouthi.
Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel imeripoti kuwa Benjamin Netanyahu ndiye aliyeagiza shambulizi hilo dhidi ya Yemen siku ya Alhamisi, wakati akiwa safarini kuelekea New York.
Ofisi hiyo iliongeza kuwa Netanyahu alikuwa akipokea taarifa za moja kwa moja kuhusu operesheni hiyo kutoka kwa Waziri wake wa Ulinzi, Mkuu wa Majeshi, na Katibu wake wa Kijeshi.
Baadaye, kundi la Houthi Ansar Allah nchini Yemen lilitangaza kuzindua kombora la kisasa la kasi kubwa linaloitwa Palestine 2 kuelekea Israel, wakidai kuwa kombora hilo limesababisha kusitishwa kwa shughuli katika Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion.
Televisheni ya Al Masirah, inayohusiana na Wahouthi, ilinukuu chanzo kutoka Idara ya Usalama na Ujasusi kikisema kuwa “uvamizi wa Israel dhidi ya Sanaa ulilengwa katika kituo cha marekebisho ya tabia (gereza) kinachosimamiwa na idara hiyo, ambacho kinahifadhi wafungwa na mahabusu.”
Hapo awali, kituo hicho cha habari kiliripoti kuhusu “uvamizi wa Israel unaolenga mji mkuu Sanaa,” uliotokea wakati huo huo na matangazo ya hotuba ya kila wiki ya kiongozi wa Wahouthi, Abdulmalik al-Houthi.
Mwandishi wa shirika la habari la AFP aliyepo Sanaa aliripoti kusikia milipuko mikubwa na kuona moshi ukipanda kutoka maeneo matatu tofauti ya jiji hilo.
Waziri wa Ulinzi wa Israel, Yisrael Katz, alituma ujumbe kupitia mtandao wa kijamii X akirejea tishio lake kwa Wahouthi, akisema: “Wahouthi, magaidi wa Yemen, wamekataa kujifunza kutoka Iran, Lebanon na Gaza sasa watalazimika kujifunza kwa njia ngumu.”
Aidha, alisisitiza kwamba, “yeyote anayehujumu Israel, atajibiwa kwa nguvu mara saba zaidi.”
Kwa upande wake, Meya wa Eilat, Eli Lankri, katika mahojiano na Kituo cha Televisheni cha 12 nchini Israel, alitoa wito wa “mashambulizi makali dhidi ya Wahouthi,” akibainisha kuwa “mashambulizi yao ya mara kwa mara yamevuruga shughuli katika bandari ya Eilat.”
Mwisho wa mwezi Agosti, shambulizi la anga la Israel lilimuua Waziri Mkuu wa Wahouthi, Ahmed Ghaleb al-Rahwi, pamoja na mawaziri na maafisa wengine tisa waliokuwa kwenye kikao mjini Sanaa.
Mapema mwezi Septemba, watu wasiopungua 46 waliuawa katika mashambulizi ya Israel yaliyolenga mji mkuu wa Yemen, Sanaa, na mkoa wa kaskazini wa Al-Jawf wakiwemo watu 38 waliouawa Sanaa ambapo vituo vya habari na taasisi zinazohusiana na Wahouthi vililengwa.
Vijana raia wawili wa Somalia wakamatwa kwa kuidharau bendera ya Kenya
Polisi nchini Kenya wamewakamata vijana wawili kwa kosa la kuidharau bendera ya taifa.
Katika mechi ya soka kati ya klabu ya Kenya na ya Somalia iliyofanyika Jumamosi iliyopita,vijana hao wanaoaminika kuwa mashabikiwa Mogadishu FC, walionekana wakiitupa chini bendera ya Kenya na kisha kuikanyaga.
Baadhi ya Wakenya walieleezea ghadhabu yao mitandaoni kuhusu kitendo hicho wakikitaja kuikosea heshima bendera ya taifa na kutaka vijana hao kukamatwa na kuchukuliwa hatua.
Siku ya Jumatano, Balozi wa Somalia nchini Kenya aliomba radhi Kuhusiana na kisa hicho lakini hata naye alilaumiwa kwa kuiweka bendera ya Kenya juu chini wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Trump asema ‘hatamruhusu’ Netanyahu kuuchukua Ukingo wa Magharibi

Rais wa Marekani Donald Trump amesema hatairuhusu Israel kuuchukua ukingo wa Magharibi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House Rais Trump amesisitiza hilo halitafanyika.
Trump, ambaye anatarajiwa kukutana na Netanyahu Jumatatu ijayo, pia amesema mpango wa kukomesha mzozo wa Gaza “unakaribia” kufikiwa.
Israel inakabiliwa na ongezeko la shinikizo la kimataifa la kutaka kukomesha vita huko Gaza na kukalia kiabavu Ukingo wa Magharibi huku wimbi la mataifa ya Magharibi yakitambua rasmi taifa huru la Palestina.
Baadhi ya wanasiasa wenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia wa serikali ya Israel wametaka Israel kutanua maeneo ya Palestina wanayoyakalia kimabavu baada ya Uingereza,Ufaransa na nchi nchi nyingine kutangaza kuitambua rasmi Palestina kama taifa.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameapa kutoruhusu kuwepo kwa taifa huru la Palestina.
Mkurugenzi wa zamani wa FBI James Comey ashitakiwa

Aliyekuwa wa shirika la upelelezi la Marekani FBI James Comey ameshitakiwa kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kwa Bunge la Marekani na kuzuia haki kutendeka.
Rais Trump alimfuta kazi Bwana Comey mnamo mwaka 2017,muda mfupi tu baada ya kuthibitika kuwa Rais huyo alikuwa anachunguzwa kuhusiana na madai kuwa Urusi iliingilia uchaguzi mkuu wa Marekani wa mwaka 2016.
Mwanasheria Mkuu wa Marekani Pam Bondi alisema katika taarifa kwamba hati ya mashtaka “inaonyesha dhamira ya Idara hii ya Haki ya kuwawajibisha wale wanaotumia vibaya nyadhifa zao kuwapotosha Warekani”.
Inaaminika kuwa mashitaka dhidi ya Comey yanahusiana na ushahidi alioutoa mbele ya kamati la Baraza la Seneti la masuala ya sheria ambapo alikanusha madai kuwa alifichua kwa vyombo vya habari taarifa nyeti kuhusu namna Urusi iliuingia uchaguzi wa Marekani.
Comey ni mkurugenzi wa kwanza wa zamani wa FBI kushtakiwa kwa uhalifu, ingawa anashikilia kuwa hajadanganya chini ya kiapo.
Ikiwa atapatikana na hatia, atakabiliwa na kifungwa cha hadi miaka mitano jela.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.