Ukitaka Mungu akutumie kwa viwango tembea katika uhalisia wako jinsi ulivyo. Usiige maisha ya wengine na kuyafanya kuwa yako. Naweza kuyapenda mafundisho ya Mwakasege lakini siwezi kuwa Mwakasege. Naweza kumpenda Prophet Jeremiah Omoto lakini siwezi kuwa Jeremiah Omoto. Mimi ni Cantona Joseph, na nikiruhusu Mungu anitumie kama Cantona Joseph hapo ndipo nitazifaidi baraka zote zilizoandaliwa kwa ajili ya Cantona. Chukua somo hili utembee nalo ili uone mabadiriko, ila kama unataka kuwa Yakobo chini ya baraka za Esau hiyo pia ni sawa, ila siku utakayoshtuka na kuzitaka baraka zako halisi itakubidi upigane miereka, na utabarikiwa ukiwa unachechemea. Na kwa binadamu wa sasa tunaokula chipsi yai, hatuna nguvu za kutosha, unaweza kubarikiwa wakati uko ICU.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.