Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Wapiga kura wamemkataa rais wa sasa Lazarus Chakwera baada ya muhula mmoja madarakani wa miaka mitano ambapo walishuhudia mgogoro mbaya mno wa kiuchumi.
Tume ya uchaguzi ya Malawi ilimtangaza Mutharika kuwa mshindi wa uchaguzi huo kwa asilimia 56 huku Chakwera akipata asilimia 33.
Awali, Bwana Chakwera alikubali kushindwa na kusema anataka kukabidhi madaraka kwa njia ya amani.
Katika hotuba yake, Chakwera alitambua matokeo ya kura za awali, jambo ambalo lilionyesha mpinzani wake Peter Mutharika alikuwa ameongoza kwa kiasi kikubwa.
“Ninajua kwamba kwa wengi wenu mliopiga kura, matokeo haya ni taswira ya nia yenu ya pamoja ya kuwa na mabadiliko ya serikali na hivyo ni sawa kukubali kushindwa kutokana na kuheshimu matakwa yenu kama raia,” aliwaambia Wamalawi.
Chakwera anasema amempigia simu Mutharika kumpongeza kwa “ushindi wake wa kihistoria”.
Alithibitisha kuwa alifika mahakamani jana kujaribu kuzuia matokeo yasitangazwe lakini akasema anakubali uamuzi wa mahakama kwamba tume ya uchaguzi lazima iendelee na kutangaza matokeo.
Chakwera pia alisema: “Wamalawi, kama mko upande wa kushindwa au kushinda, tafadhali muwe na amani.”
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.