Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda amejibu matamshi yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Katika hotuba hiyo, Rais Felix Tshisekedi kwa mara nyingine alisema amerejea vitani vikosi vya serikali yake vinapambana na waasi wa M23 mashariki mwa Congo.
Tshisekedi alitangaza kwamba kinachofanywa kwa watu wa Kivu Kusini na Kaskazini ni ”mauaji ya halaiki”.
Waziri Olivier Nduhungirehe, katika mahojiano na BBC, alisema kuwa Rais Tshisekedi ‘hajui kuhusu mauaji ya kimbari.’
Rais Tshisekedi pia aliishutumu Rwanda kwa kutoheshimu azimio la Umoja wa Mataifa na makubaliano yaliyotiwa saini mjini Washington, na kuiamuru kuwaondoa wanajeshi wake katika ardhi ya Congo, na kuacha kutoa msaada kwa M23.
Lakini Olivier Nduhungirehe anasema licha ya ombi lake bado anafanya kazi na FDLR ambayo alitakiwa kuiondoa kwanza ili Rwanda nayo iondoe hatua za kiusalama ilizoziweka kwa kundi hilo. Anamtaka Tschesekedi asome tena Mkataba wa Washington kwa umakini.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.