Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

January 20, mwaka 1961 baada ya John F. Kennedy kuapishwa kama Rais wa marekani…
Aliongea kwa dakika 14 zilizoleta falsafa mpya kabisa kuhusu swali ambalo kila mtu anatakiwa kujiuliza kila siku anapoamka.
Kupitia sentensi yake muhimu sana ya “Usijiulize nchi yako itakufanyia nini, jiulize wewe utaifanyia nini nchi yako”…
Ask not what your country will do for you but what will you do for your country.
Ilileta tafsiri mpya ya makundi mawili ya watu kwenye kila Taifa.
Moja ni wale ambao wanaamini bila kujali nafasi waliyonayo, elimu yao n.k
Wanaamini wana fursa ya kuchangia Katika mafanikio ya taifa lao kwa kupitia kilicho ndani ya uwezo wao.
Kuifanyia nchi yako kitu ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii, kuwa mwaminifu, kusimamia haki…
Kuwatia moyo wanaofanya mambo mazuri kwa Taifa…
Kuwa na ushawishi chanya kwenye jamii, kukemea uovu n.k
Mbili ni wale ambao kila wanapoamka wanaanza kutafuta mtu wa kumlaumu…
Na kuonyesha kuwa hakuna chochote wanachoweza kufanya kuchangia mabadiliko katika nchi.
Wanaamini katika kubebesha lawama wazazi, marafiki, mabosi wao, viongozi n.k
Mara zote huamini kuwa hawana nguvu ya kuleta mabadiliko kwao wenyewe na kwa jamii inayowazunguka.
Kuna wakati unaweza kudhania kuwa unachofanya kwa ajili ya nchi yako ni bure, la hasha: Kila mbegu njema itaota.
Ndio maana Biblia inasema “MSICHOKE kutenda MEMA, kwani mtavuna kwa wakati wake”.
Hata kama kila mtu haoni THAMANI ya unachofanya au kinaonekana ni KIDOGO…
Wewe amua kuendelea kufanya kwa faida ya nchi yako na kizazi chako.
Leo utafanya JEMA gani kwa nchi yako?
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.