Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kwenye mashindano ya Olimpiki ya mwaka 2004 mkanada Perdita Felicien alikuwa ndiye mtu anayetarajiwa…
…kushinda medali ya dhahabu kwenye mbio za mita 100 za kuruka vizuizi.
Hii ilitokana na sababu mbili…
Moja ni kwa sababu katika mashindano yaliyopita, alikuwa ndiye mshindi nambari moja.
Ya pili ni kwa sababu katika miaka minne alikuwa yuko fit bila jeraha akijiandaa na mashindano hayo.
Anasema kuwa alikuwa anafanya mazoezi kwa muda wote wa miaka 4…
Kwa muda wa masaa sita kila siku katika siku 6 za wiki…
….na alipumzika siku moja tu katika wiki.
Hata hivyo siku ya mashindano, alianguka alipoanza kuruka kwenye kikwazo cha kwanza tu.
Sio tu yeye alishangaa na kupata huzuni…
…hata watazamaji na mashabiki iliwashangaza sana.
Alipokuwa akiongea na waandishi wa habari…
…badala ya kulaumu na kulalamikia kitu chochote akasema…
…“hata mimi nimeshangaa kwa nini imetokea hivyo.
Ila najua kila kitu kina sababu.
Hii imenipa njaa zaidi ya kushinda na naahidi nitaongeza bidii ya…
…mazoezi na baada ya miaka minne nitarudi tena uwanjani ili niipate dhahabu yangu”.
Hii ndio tofauti ya wanaoshindwa na wanaoshinda.
Ukishindwa mara moja haimaanishi UMEFELI MAISHA.
Usikate tamaa, Jipange UPYA.
Ulifeli biashara, mahusiano yalifeli, Ulipoteza mtaji, Ulifukuzwa kazi.
USIHITIMISHE KUWA NDIO UMEFIKA MWISHO.
Jipange UPYA, Unaweza kufanikiwa tena.
Leo, dhamiria KUINUKA UPYA BAADA YA KUANGUKA.
Inawezekana kutimiza ndoto yako.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.