Uvumilivu ni kazi Ngumu sana..

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Aliyewahi kuwa spika wa bunge la marekani ambaye pia ni mwandishi wa vitabu….

Newt Gingrich aliwahi kusema…

“Perseverence is the hard work you do after you get tired of doing the hard work you arleady did”…

Uvumilivu unauonyesha pale ambapo unaamua kufanya kwa bidii zaidi baada ya…

Kuwa umechoka sana kwa sababu umefanya kwa bidii sana kabla ya hapo.

Moja ya changamoto ambayo lazima ukabiliane nayo kila siku ni ile hali ya…

“Self-Justification” kwa nini usiendelee kufanya.

Hii ni ile hali ambapo mtu anajitengenezea uhalali wa kutofanya kitu fulani…

Kwa sababu ambazo ameridhika nazo na anaamini kila atakayezisikia…

Ataona ni halali kwake kutoendelea kufanya.

Mara nyingi watu waliofika hatua hii huwa wanasema…

“Yaani nimejitahidi sana hata wewe unajua, kwa sasa nimefika mwisho”.

Ukiwaangalia na kufuatilia utaona kuna ukweli fulani na utawaonea huruma.

Kuna mwingine atakuambia nimeweka pesa zangu nyingi na nimepoteza na ni kweli kabisa.

Kuna mwingine atasema nimejaribu sana kutafuta fursa lakini naona imshindikana.

Na ni kweli utakuta ametuma maombi sehemu nyingi na ametafuta watu wengi.

Unachotakiwa kujua ni kuwa “HAKUNA KILELE CHA MWISHO KATIKA BIDII”.

Kwa mujibu wa Gingrich, pale unapojiona kuwa UMEFIKA MWISHO wa bidii yako…

Inatakiwa iwe ndio mwanzo wa BIDII MPYA.

Je, kuna eneo ambalo umejifanyia “Self-justification”?

Leo ni wakati wa kuweka juhudi ya ziada kwa sababu mafanikio yako yamekaribia sana.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment