Biblia inaelezea kwamba, Kuna wakati Mtume Paulo alimkemea Mtume Petro kwa sababu ya unafiki wa kuwatenga watu wa mataifa pale alipowaona wayahudi (Wagalatia 2:11-21).
Petro alikuwa ni mtu mzima kiumri anaemzidi Paulo miaka mingi, lakini pia alikuwa ni miongoni mwa mitume waliohasisi imani hii wakiwa na Bwana Yesu Kristo , lakini kama hilo halitoshi bado alikuwa ndiyo mtume mkuu ambaye Yesu alimkabidhi kanisa.
Lakini pamoja na nafsi kubwa aliyokuwa nayo, ki uongozi, ki umri, na ki uzoefu bado tunaona Petro hakasiliki kwa ajili ya maonyo haya, zaidi ya yote kwenye waraka nyaraka zake utaona akimuelezea Paulo kama mtu mwenye hekima ambayo kama hauna elimu ya kutosha juu ya imani unaweza usimuelewe kabisa (2 Petro 3:15-16).
Unyenyekevu huu umepotea sana kwenye kanisa hili la leo, maaskofu wengi wana kiburi cha kujiona kama wao ndiyo wanafaa kuwakemea wengine lakini wao hawastahili kukemewa.
Yaani leo ni rahisi sana kusimama na kumuomba raisi na mkuu wa mkoa wawakamate manabii na mitume wanaoendesha huduma za maombi kwa kutumia maji, sabuni na mafuta, lakini wao ukiwakumbusha jinsi walivyochukua pesa za watu katika njia ya kutatanisha wanaanza kuhisi kama wamevunjiwa heshima.
Leo hii askofu akihubiri mambo ya siasa madhabahuni, ukimuonya anakuwa mkali anahisi kama amekosewa adabu.
Swali langu kwao ni hili, Je! Ni wao tu ndiyo wana haki ya kuonya na kukemea lakini wao hawapaswi kukemewa?
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.