Chama tawala chadai kulikuwepo na wizi wa kura

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Nchini Malawi, Chama tawala cha Rais Lazarus Chakwera kinadai kuwa kulikuwa na wizi wa kura katika uchaguzi wa wiki iliyopita huku chama hicho kikidai kuwa na ushaihidi wa kutosha wa kudhibitisha hilo.

Lazarus Chakwera ambaye chama chake kinadai kwamba uchaguzi wa urais uligubikiwa na dosari.
Lazarus Chakwera ambaye chama chake kinadai kwamba uchaguzi wa urais uligubikiwa na dosari. AFP – AMOS GUMULIRA

Kulingana na  matoeko ya awaili ya uchaguzi uliofanyika tarehe 16 mwezi huu, Chama cha Malawi Congress Party MCP kimeonekana kuzoa idadi ndogo ya kura kutoka kwa baadhi ya wilaya ambazo tayari hesabu zimekamilika.

Mgombea mwenza wa MCP Vitumbiko Mumba amesema kuwa wana ushahidi kwamba baadhi ya watu walikuwa wanajaza karatasi za kupigia kura kwenye masanduku ya kupigia kura huku akisema kuwa matokeo ya awali hayalingani na takwimu zilizotangazwa katika kituo cha kujumlisha kura.

Aidha MCP imewasilisha malalamiko kwa Tume ya Uchaguzi ya Malawi wakati ambapo Chama cha Democratic Progressive Party DPP kilikariri kuwa hesabu zake zilionyesha kuwa mgombea wake wa urais Peter Mutharika anaongoza kura hizo kwa sasa.

Karatasi la kupiga kura wakati wa uchaguzi nchini Malawi
Karatasi la kupiga kura wakati wa uchaguzi nchini Malawi Reuters – Stringer

Baada ya MCP kudai Ijumaa kuwa kulikuwa na dosari katika upigaji kura, polisi walitangaza kukamatwa kwa wafanyikazi wanane wa kuingiza data.

Rais Lazarus Chakwera aliingia madarakani katika marudio ya uchaguzi 2020 baada ya uchaguzi wa 2019 kufutwa kwa sababu ya udanganyifu.

Tume ya uchaguzi nchini humo  ina hadi Jumatano kutoa matokeo ya mwisho ya kura ya urais.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment