MAMBO 10 HATARI YANAYOWEZA KUANGUSHA BIASHARA YAKO.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Wafanyabiashara wengi hawafi kwa sababu ya kukosa wateja, bali kwa sababu ya makosa ya msingi ambayo hayarekebishwi mapema.

Kwa uhalisia wa Tanzania, anguko kubwa la biashara nyingi lipo kwenye maeneo haya makuu:

1.Kukosa Uvumilivu na Nidhamu.

Wengi wanataka matokeo ya haraka.

Utafiti unaonyesha inachukua miaka 3–5 biashara kukomaa.

Kufunga biashara baada ya miezi sita bila matokeo ni kosa kubwa.

….

2.Kukosa Maarifa ya biashara,Kisheria na Taratibu Zake.

Kutokuifahamu biashara kwa undani ni kosa kubwa sana..

Kutojua sheria za kodi, leseni na vibali.TRA, OSHA, au halmashauri ikikufungia, biashara inakufa ghafla.

Mfano unaweza kufungiwa ghafla kwa sababu ya kutolipa kodi au kutokuwa na cheti cha fire.

3.Kutojua Watu Sahihi wa Kushirikiana Nao.

Biashara nyingi huanguka kwa sababu ya watu wasio sahihi.Mshirika asiye na maadili, mfanyakazi mwizi, au timu isiyo na commitment.

Mfano utakuta mtu anashirikiana na ndugu kwa “kuamini damu ni nzito” bila mkataba wa kibiashara au ujuzi wa biashara. Mwisho wake ni migogoro na anguko.

….

4.Kukosa Ubunifu na Kubadilika.

Soko hubadilika kila siku, teknolojia inakuja na mitindo mipya.Wengi wanashikilia njia za zamani na kukataa kujaribu mbinu mpya.

Mfano utakuta duka linaendelea kuuza tu kwa wateja wa mtaani, bila kutumia WhatsApp Business, TikTok, au platforms zingine za kidigitali.

5.Kutokujua Hesabu na Mzunguko wa Fedha .

Pesa ya biashara kuchanganywa na pesa binafsi.

Kukosa uelewa wa tofauti kati ya faida, mtaji na mapato. Matokeo: biashara ina mauzo, lakini haina ukuaji.

Mfano anaingiza milioni 5 kwa mwezi, lakini kila mara kuongeza stock anatoka mfukoni binafsi. Hii inaua ukuaji.

6.Kutegemea Mawazo, Siyo Data

Kufungua biashara kwa kuiga bila utafiti wa soko.Tafiti zinaonyesha 42% ya biashara duniani hufa kwa sababu bidhaa hazihitajiki sokoni.

Mfano wa Tanzania: kufungua stationary au saloon kwa sababu “Fetty anauza sana sokoni” bila kujua demand halisi ya eneo.

….

7. Kukosa Mfumo.

Biashara ikimtegemea mtu mmoja pekee, ikikosa mfumo, ikimfunga mmiliki.

Mfumo = accounting, stock control, sales tracking, marketing system.

Mfano maduka mengi ya Mangi hubaki duka lile lile miaka 10, bila kukua.

Kuna mifumo ya kisasa kama THL Accounting ambayo inasaidia kupunguza tatizo hili.

8. Kutumia Mtaji Vibaya.

Faida na mtaji kutumika kwa matumizi ya kibinafsi kama vile magari, nguo, sherehe.Hii inajulikana kama “kula mtaji”.

Mfano biashara ina faida ya 2M kwa mwezi, lakini mmiliki anakimbilia kununua RANGE ROVER yenye namba za jina lake.

9.Kukosa Kujitofautisha.

Wengi wanauza huduma au bidhaa kwa namna ile ile.Hii inaleta ushindani wa bei (price war).Mwisho wa siku wote mnashindana kushuka bei na mnaishia hasara. Ukijitofautisha sokoni inakusaidia kupata matokeo makubwa.

10.Kutokuweka Mikakati ya Uuzaji.

Biashara nyingi hazitangazwi.Kutegemea “marafiki na ndugu” ni kosa kubwa.

Kukosa brand identity, social media strategy, au mfumo wa kurudisha wateja (customer retention).Hii inafanya biashara isimame tu pale ilipo bila kupiga hatua.

..

Unatakiwa kujua kuwa biashara haianguki ghafla huanguka kwa hatua ndogo ndogo za makosa haya.

Kama uko kwenye biashara, hakikisha unajipima kwenye haya maeneo 10 na kufanya marekebisho mapema.

Ni jambo gani ambalo bado linakusumbua katika biashara kati ya haya mambo 10?

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment