Bila Kufanya Hili Huwezi Kuanzisha Biashara Yenye Mafanikio…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Fanya utafiti wa soko lako na mapema..

Hapa ndipo wafanyabiashara wengi hufeli.

Hawajui kuwa kanuni ya soko inasema “Usianze biashara unayoitaka wewe, Bali anzisha biashara inayoitajika na wateja. Utajua hili kwa kufanya utafiti..

HATUA ZA KUCHAMBUA SOKO..

1. Tambua matatizo na mahitaji ya watu karibu yako

Biashara nzuri huanza kwa kutatua tatizo.

Kwa mfano

✍️Mtaa hauna sehemu ya huduma ya gesi → fursa ya biashara ya gesi.

✍️Watu wanaenda mbali kutengeneza printing → fursa ya copy center.

✍️Sehemu haina genge → fursa ya genge nzuri.

2. Fuatilia mwenendo wa matumizi ya Watanzania,Wakenya au Waganda.

Tumia takwimu na ripoti rasmi ili kubaini wapi matumizi yanaongezeka.

Mfano tumia takwimu hizi..

✍️Ripoti ya BOT & TCRA: Matumizi ya intaneti yanaongezeka → fursa ya biashara mtandaoni (online business).

✍️Takwimu: Familia mjini hutumia 65% ya mapato kwenye chakula → biashara za chakula ni “never dying market.”

Kuongezeka kwa vijana mijini → fursa ya fashion, saluni, na burudani.

3. Chunguza Washindani (Competition Analysis)

👉 Usianze bila kujua nani tayari yupo sokoni.

Ni wangapi? Wanatoa huduma vipi (bei, ubora, speed, location)?

Je, kuna mapengo (gaps) unaweza kuziba?

Kwa mfano kama saluni zote jirani zinakata nywele tu, unaweza kuongeza huduma ya massage au pedicure → differentiation.

Kama mgahawa jirani anauza chakula ghali, unaweza kuja na bei nafuu au huduma ya delivery.

4. Uliza wateja kabla ya kuanza (Customer Validation)

👉 Usihangaike na makisio yako, uliza wat hiu moja kwa moja.

.

Kwa mfano kabla ya kufungua mgahawa, uliza watu 20 jirani yako..

.

Je, mngependa mgahawa mpya? Ni huduma gani zingewavuta zaidi?Bei gani mngeona ni nafuu?

.

Faida unaanza na wateja tayari wamesema wanataka huduma yako.

5. Pima ukubwa wa soko (Market Size)

👉 Angalia idadi ya wateja watakaokuwezesha kupata faida.

Je, eneo lako lina watu wa kutosha? Ni asilimia ngapi ya watu watakuwa wateja wako?Je, soko litaendelea kukua? Kwa mfano..

Eneo lina watu 10,000 → hata 5% (500 watu) wakiwa wateja wa mara kwa mara, biashara yako itasimama.

6. Angalia mwenendo wa muda mrefu

👉 Je, biashara hii ni ya msimu au inaweza kudumu?

Biashara za chakula, afya, elimu, makazi → hazifi.

Biashara za fashion, electronics → zinahitaji ufuatiliaji wa mitindo kila mara.

Faida za kufanya utafiti.

✅Inakusaidia kubaini tatizo la eneo husika..

✅Inasaidia kujua washindani wako udhaifu na ubora wao.

✅ Inasaidia kujua wateja wako vizuri umri wao,jinsia zao, uwezo wao.

✅ Inasaidia kujua sehemu sahihi ya chimbo la kujumua mzigo. Sehemu yenye bei ndogo na yenye bidhaa nzuri.

Usiingie kwenye biashara kwa kusikia tu kuwa inalipa ila unapaswa kujiridhisha kwa kufanya utafiti wa soko lako.

Wewe unapata ugumu gani kufanya utafiti.?

Andika hapa chini kwenye comment ili niweze kukusaidia..

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment