Viinite kugawanywa kwa familia: Mahakama ya Ukraine yawapa wazazi wa marehemu nusu ya viinitete

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

g
Maelezo ya picha,Kesi ambayo haijawahi kutokea katika mahakama ya Dnipro kuna uwezekano mkubwa itaendelea

Kashfa ilizuka huko Dnipro nchini Ukraine kuhusu uamuzi wa mahakama kuhusu viini-tete vya marehemu vilivyohifadhiwa.

Kinyume na mapenzi ya mke wa marehemu, mahakama iliamua kuhamisha nusu ya viinitete hivyo kwa babu na bibi wa watoto watarajiwa na kumwachia mjane wa marehemu nusu nyingine.

Mwanamke huyo mchanga anapanga kukata rufaa dhidi ya uamuzi huu kwa mahakama za juu zaidi, na wataalamu wanasema ni uamuzi wa mahakama ambao haujawahi kushuhudiwa ambao unaweza kuwa na matokeo mabaya katika siku zijazo.

Kesi hii imeendelea kwa takriban miaka miwili, lakini inaonekana kwamba haitaishia kwa uamuzi huu.

Viinitete na kusaidiwa kubeba ujauzito

Wanandoa hao wachanga walikuwa wakifanyiwa matibabu ya utasa na walikubali kurutubishwa kwa njia ya uzazi. Kwa hili, madaktari waliwasaidia kupata viinitete sita.

Hatahivyo kwa bahati mbaya mwanamume huyo, Oleksandr Kuzmenko, alikufa.

Kama mke wake Anastasia Kuzmenko alisema, baada ya janga hili, hakuwa na swali la uhamishaji wa kiinitete haraka, kwani alikuwa akipitia kifo cha mpendwa wake kwani alikuwa amechoka, na alikuwa akimeza dawa.

Anastasia aliwaambia wazazi wa mumewe kwamba hatapanga ujauzito kwa mwaka mmoja baada ya kifo chake.

Lakini hawakutaka kungoja kwa muda mrefu na wakamruhusu akubali kuolewa. Anastasia alikataa, kwa hivyo walienda mahakamani kudai wachukue viinitete.

“Mahakama iliamua kuwapa baadhi ya viinitete vyangu jamaa za mume wangu. Sikuweza kufikiria hili hata katika ndoto yangu mbaya zaidi,” Anastasia Kuzmenko alijibu .

Israel yawaondoa kwa nguvu wakazi wa kusini mwa Syria – Human Rights Watch

g
Maelezo ya picha,Baada ya kuanguka kwa utawala wa Assad, Israel ilitangaza kuudhibiti Mlima Hermoni

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limevishutumu vikosi vya Israel kwa kuwahamisha wakazi wa vijiji vya kusini mwa Syria kwa nguvu.

Haya yanajiri huku televisheni ya taifa ya Syria ikiripoti kuwa wanajeshi wa Israel waliwakamata watu wanne katika Mkoa wa Quneitra kusini mwa Syria siku ya Jumatano. Jeshi la Israel lilisema lilihusika katika “shughuli za kigaidi.”

Ripoti ya Human Rights Watch ilisema kuwa “vikosi vya Israel, ambavyo vimeteka maeneo ya kusini mwa Syria tangu Desemba 2024, vimefanya msururu wa dhuluma dhidi ya idadi ya watu.”

Shirika hilo lilinukuu jeshi la Israel likisema kuwa shughuli zake “zinafuata sheria za kimataifa” na kwamba zinatekelezwa kusini mwa Syria “kuwalinda raia wa Taifa la Israel.”

“Majeshi ya Israel yalinyakua na kubomoa nyumba, kuwanyima wakazi mali na riziki zao, na kuwaweka kizuizini kiholela na kuwahamisha wakazi hadi Israel,” Human Rights Watch ilisema katika ripoti yake.

Shirika hilo lilisema liliwahoji wakazi wa eneo hilo, likahakiki picha na video, na kuchanganua taswira za satelaiti.

Likijibu swali kutoka kwa ofisi ya AFP mjini Jerusalem, Jeshi la Israel, lilisema kuwa vikosi vyake vimewakamata usiku kucha “idadi ya watu wanaoshukiwa kuhusika na shughuli za kigaidi zinazolenga (majeshi yake) katika maeneo kadhaa ya Syria… Washukiwa hao walihamishwa kwa mahojiano zaidi ndani ya ardhi ya Israel.”

Familia za waathiriwa wa ajali ya Air India zashitaki kampuni za Boeing na Honeywell

.

Familia za abiria wanne waliofariki kwenye ndege ya Air India iliyoanguka mwezi Juni wamewasilisha kesi nchini Marekani dhidi ya kampuni ya ndege ya Boeing na kampuni ya kutengeneza vipuri vya ndege ya Honeywell, wakizituhumu kampuni hizo kwa uzembe.

Kesi hiyo iliyowasilishwa Jumanne, na iliyoonekana na BBC, ilisema swichi zenye hitilafu za mafuta zilisababisha ajali hiyo na kuzishutumu kampuni hizo kwa “kutofanya lolote” licha ya kufahamu hatari za muundo wa ndege hiyo.

Ndege ya Air India 171 iliyokuwa ikielekea London Gatwick, Boeing 787, ilianguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka Ahmedabad na kuua watu 260.

Swichi za mafuta zimekuwa angalizo kwa wachunguzi baada ya uchunguzi wa awali kubaini kuwa mafuta kwa injini yalikatika muda mfupi baada ya ndege kupaa.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment