‘Ushahidi wa kisayansi’ kutolewa kuthibitisha kuwa mke wa Rais Macron ni mwanamke, wakili asema

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Emmanuel Macron na mkewe, Brigitte, wanapanga kuwasilisha ushahidi wa picha na kisayansi kwa mahakama ya Marekani kuthibitisha Bi Macron ni mwanamke.

Wakili wao anasema Rais wa Ufaransa na Bi Macron watawasilisha nyaraka hizo katika kesi ya kumharibia sifa dhidi ya mfuasi wa mrengo wa kulia Candace Owens baada ya kuendeleza imani yake kwamba Brigitte Macron alizaliwa mwanaume.

Mawakili wa Bi Owens wamejibu wakionyesha kuwa madai ya familia ya Macron ni ya uwongo.

Akizungumza na podikasti ya ‘BBC Fame Under Fire’, wakili wa familia ya Macron katika kesi hiyo, Tom Clare, alisema Bi Macron amechukulia madai hayo kuwa “ya kuhuzunisha sana” na yalikuwa “usumbufu” kwa rais wa Ufaransa.

Familia za waathiriwa wa ajali ya Air India zashitaki kampuni za Boeing na Honeywell

.

Familia za abiria wanne waliofariki kwenye ndege ya Air India iliyoanguka mwezi Juni wamewasilisha kesi nchini Marekani dhidi ya kampuni ya ndege ya Boeing na kampuni ya kutengeneza vipuri vya ndege ya Honeywell, wakizituhumu kampuni hizo kwa uzembe.

Kesi hiyo iliyowasilishwa Jumanne, na iliyoonekana na BBC, ilisema swichi zenye hitilafu za mafuta zilisababisha ajali hiyo na kuzishutumu kampuni hizo kwa “kutofanya lolote” licha ya kufahamu hatari za muundo wa ndege hiyo.

Ndege ya Air India 171 iliyokuwa ikielekea London Gatwick, Boeing 787, ilianguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka Ahmedabad na kuua watu 260.

Swichi za mafuta zimekuwa angalizo kwa wachunguzi baada ya uchunguzi wa awali kubaini kuwa mafuta kwa injini yalikatika muda mfupi baada ya ndege kupaa.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment