Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, limesema serikali duniani kote, hasa katika mataifa yenye nguvu ikiwemo Marekani na nchi za Ulaya, yanaendelea kudhoofisha mkataba wa kimataifa wa mwaka 1951 kuhusu wakimbizi na waomba hifadhi, hatua inayotishia uwepo wake.
I

Katika taarifa yake, UNHCR imeonya kwamba huenda makubaliano haya yanayoweka wazi majukumu ya mataifakwa wakimbizi yakapuuzwa, ambapo kulingana na Umoja wa mataifa, nchi zimetupilia mbali maombi ya waomba hifadhi na wale wanaokimbia hali ngumu kwenye nchi zao.
Utawala wa Rais Trump na ule wa nchi nyengine za Ulaya wamekuwa wakiwafukuza wakimbizi na waomba hifadhi, baadhi yao wakipelekwa katika mataifa ya Afrika chini ya makubaliano na nchi za serikali husika.

Licha ya kwamba nchi kama Marekani zimetangaza sheria kali dhidi ya uhamiaji, Ugiriki kwa upande wake imesitisha mpango wa kuwapokea waomba hifadhi, hali inayotishia usalama wao.
Mzozo wa ufadhili duniani umewaathiri zaidi ya watu Milioni 122 waliopoteza makazi yao kutokana na mizozo ya ndani au wale wanaokimbilia katika mataifa ya kigeni kwa ajili ya usalama wao.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.