Vifaru vya Israel vyaingia katika eneo kubwa la makazi la Gaza

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Wakaazi wa eneo la Gaza na mashuhuda wanasema makumi ya vifaru na magari ya kijeshi ya Israel yameingia katika wilaya kubwa ya makazi ya mji wa Gaza, katika siku ya pili ya mashambulizi ya ardhini ya Israel yenye lengo la kuteka eneo hilo.

Kanda za video zinaonyesha vifaru, tingatinga na wafanyakazi wenye silaha zikisonga pembezoni mwa Sheikh Radwan, kaskazini mwa jiji la Gaza.

Mawingu mazito ya moshi yanaweza kuonekana huku vikosi vya Israeli vikifyatua makombora ya risasi na mabomu ya moshi ili kuficha ujio wao.

Wilaya ya Sheikh Radwan ilikuwa makazi ya makumi ya maelfu ya watu kabla ya vita na inachukuliwa kuwa mojawapo ya maeneo yenye wakazi wengi zaidi wa jiji hilo.

Israel inasema lengo la mashambulizi yake katika mji wa Gaza ni kuwaachia huru mateka wanaoshikiliwa na Hamas na kuwashinda hadi wapiganaji 3,000 katika kile inachoeleza kama “ngome ya mwisho” ya kundi hilo – lakini operesheni hiyo imeshutumiwa kimataifa.

Trump asuburiwa kwenye mkutano wa UN huku mizozo ya Gaza, Ukraine ikizidi kutokota

.

Viongozi wa dunia watakusanyika mjini New York wiki ijayo kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Rais wa Marekani Donald Trump anasubiriwa kwa hamu huku mzozo wa Gaza na Ukraine ukiendelea kutanuka, na hivyo kuongezeka hamu ya mataifa ya Magharibi ya kutambua taifa la Palestina huku mivutano ya nyuklia na Iran ikiendelea.

“Tunakusanyika kukiwa na hali ya msukosuko – hata ambayo hayajajulikana,” Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema wiki moja kabla ya baraza hilo la wanachama 193 kuwa mwenyeji wa siku sita za hotuba za takriban viongozi 150 wa nchi au serikali pamoja na mawaziri kadhaa zaidi.

Kitakachopewa kipaumbele kwenye Baraza Kuu la 80 la mwaka huu, atakuwa Trump ambaye anatoa wito wa kupunguzwa ufadhili wa Marekani kwa Umoja wa Mataifa, alisimamisha ushirikiano wa Marekani na Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa, akaongeza usitishaji wa ufadhili wa shirika la misaada la Palestina UNRWA na kujiondoa kwenye shirika la Umoja wa Mataifa la utamaduni UNESCO. Pia ametangaza mipango ya kujiondoa kwenye makubaliano ya hali ya hewa ya Paris na Shirika la Afya Duniani.

Trump atazungumza siku ya Jumanne, miezi minane katika kipindi chake cha muhula wa pili ambao umetawaliwa na upunguzaji wa kiasi kikubwa wa misaada ya kigeni wa Marekani ambao umesababisha athari za kibinadamu duniani na kuzua maswali kuhusu mustakabali wa Umoja wa Mataifa, na kumfanya Guterres kujaribu kupunguza gharama na kuboresha ufanisi.

Trump anaelezea Umoja wa Mataifa kuwa na “uwezo mkubwa” lakini anasema inabidi “kuchukua hatua ya pamoja.” Amedumisha msimamo ule ule wa tahadhari juu ya ushirikiano wa pande nyingi ambao ulikuwa kauli yake katika muhula wake wa kwanza kutoka 2017 hadi 2021 na pia alishutumu shirika hilo kwa kushindwa kumsaidia kujaribu kuleta amani katika migogoro mbalimbali.

“UN ina juhudi kubwa sana katika upatanishi wa amani … lakini hatuna…viboko,” Guterres alisema.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ndilo chombo pekee cha Umoja wa Mataifa kinachoweza kuweka vikwazo, lakini limekwama kwenye mizozo ya Gaza na Ukraine kwa sababu Marekani na Urusi zina mamlaka ya kura ya turufu.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment