Usimhukumu samaki kupanda juu ya Mti;

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kama utamhukumu Samaki kwa kushindwa

kupanda juu ya mti…

…Basi samaki ataishi Maisha yake yote akiamini kwamba HANA AKILI.

– Albert Einstein

Kila mtu ni “GENIUS” katika eneo fulani katika maisha yake.

Hakuna mtu ambaye hana uwezo kabisa wa kufika kilele cha mafanikio katika maisha yake.

Hii inamaanisha kuwa kama hauwezi kufanya kitu fulani…

…SIO Hitimisho kwamba hautaweza kufanya kitu kingine chochote katika Maisha yako.

Kuna eneo ambalo ukiligundua na ukaamua kuwekeza litakufanya uwe WA TOFAUTI SANA.

Hapa ndio utaelewa kwa nini kuna watu ambao HAWAKUWA wanafanya vizuri shuleni lakini…

…kwenye maisha waliamua kufanya kitu fulani na WAKAFANIKIWA SANA.

Hii ni kwa sababu kuna aina za “UGENIUS” ambazo mfumo wa kawaida wa shule hauwezi Kuzijua na Kuzipima.

Kama LEO ningeambiwa nirudi nyuma nichague…

…Masomo na Kozi za kufanya kwa ufahamu nilio nao sasa hivi nina uhakika ningefanya maamuzi TOFAUTI KABISA.

Kila mtu ana uwezo mkubwa sana wa kipekee ndani yake (CORE GENIUS).

Uwezo ambao kama akiugundua anaweza kufanya mambo MAKUBWA SANA.

Katika aina 8 za ugenius ambazo mtu anazo…

…kwa bahati mbaya mfumo wa shule umejikita katika MBILI (2) Tu!.

Matokeo yake, watu wengi hadi wanapoondoka duniani wanaishia kufanya vitu wasivyopaswa kufanya na uwezo wao haujulikani kabisa.

Wewe USIWE MMOJA WAO!

Ninachofanya leo ni sehemu ya kugundua “Core Genius” yangu iliyonisaidia kujua kitu sahihi cha kufanya nje ya kile nilichosomea shuleni.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment