Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva, ametetea huku iliyomkuta mtangulizi wake Jair Bolsonaro ya kuhukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka 27 jela kwa kupanga mapinduzi.
Katika maoni yake yalichochapishwa katika gazeti la New York Times, Lula amekosoa matamshi ya Rais wa Marekani Donald Trump kuwa kesi hiyo ilikuwa ni ya kisiasa na kusema ni “uamuzi wa kihistoria ambao unalinda taasisi zetu na utawala wa sheria katika demokrasia”.
Kiongozi huyo wa Brazil ameandika makala hiyo ili kuanzisha mazungumzo ya wazi na ya kweli na Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye ameweka ushuru wa asilimia 50 kwa bidhaa za Brazil zinazoingia Marekani.
Lula ameliita ongezeko hilo la ushuru “sio tu kwamba ni potofu lakini lisilo na mantiki.”
Mahusiano yamekuwa ya mvutano kati ya Marekani na Brazil katika miezi ya hivi karibuni, tofauti kabisa na uhusiano wa Trump na Jair Bolsonaro alipokuwa rais.
Bolsonaro mara nyingi alionyesha kuvutiwa kwake na Trump, ambaye alimkaribisha katika jumba lake la kifakhari la kifakhari la Mar-a Lago kwa ajili ya mapumziko mwaka 2020.
Lula, kiongozi wa mrengo wa kushoto, anayejulikana kwa kunyoosha, hakumunya maneno yake katika makala yake ya New York Times.
Amesema kuwa katika kipindi cha miaka 15 iliyopita Marekani “imekusanya ziada ya dola bilioni 410 (£302bn) katika biashara na huduma baina ya nchi hizo mbili,” na kusema uamuzi wa kuongeza ushuru unaweza kuwa wa kisiasa tu.
“Serikali ya Marekani inatumia ushuru na vikwazo kuzuia kutoadhibiwa kwa Rais wa zamani Jair Bolsonaro,” Lula aliandika, akimaanisha vikwazo ambavyo Marekani imeviweka kwa jaji wa Mahakama ya Juu ambaye aliongoza kesi dhidi ya Bolsonaro.
Kesi hiyo ilikamilika Alhamisi wakati majaji wanne kati ya watano wa Mahakama ya Juu, walipompata hatia ya mashtaka yote matano aliyokuwa akikabiliwa nayo.
Bolsonaro amehukumiwa kifungo cha miaka 27 na miezi 3 jela – hukumu ambayo mawakili wake wanasema watakata rufaa.
Trump amesema hukumu hiyo “ya kushangaza sana” na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alitangaza kwamba Marekani “itajibu ipasavyo kuhusu kuhusu hiyio.”
Katika makala yake ya New York Times, Lula alisisitiza kuwa kesi hiyo “si ya kisiasa”.
“Hukumu hiyo ilikuwa matokeo ya kesi kwa mujibu wa Katiba ya Brazili ya 1988, iliyotungwa baada ya miongo miwili ya mapambano dhidi ya udikteta wa kijeshi,” aliandika, akiwakumbusha wasomaji kwamba demokrasia ya Brazili ilirejeshwa mwaka 1985 baada ya miaka 20 ya utawala wa kijeshi.
Lula pia alikanusha shutuma za utawala wa Trump kwamba mfumo wa haki wa Brazil unalenga na kukandamiza makampuni ya teknolojia ya Marekani.
Rais wa Brazil amesema mahakama za nchi yake zilikuwa sahihi kudhibiti intaneti na makampuni ya Marekani hayakutendwa vibaya.
Alihitimisha makala yake kwa kumhutubia Rais Trump moja kwa moja, akimwambia kwamba Brazil bado iko tayari kujadili “chochote ambacho kinaweza kuleta manufaa kwa pande zote”, lakini akamuonya Trump kwamba “demokrasia na uhuru wa Brazil havitajadiliwa.”
Rubio anakutana na Netanyahu kujadili shambulio la Israel dhidi ya Qatar

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio anakutana na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu jijini Jerusalem, huku shambulio la Israel nchini Qatar likitarajiwa kuwa ajenda kuu.
Shambulio la wiki jana, ambalo lililenga viongozi wakuu wa Hamas katika nchi ambayo ni mshirika wa karibu wa Marekani, lilibua hasira kimataifa na kukosolewa na Rais Donald Trump.
Rubio awali alisema: “Ni wazi hatujafurahishwa na hilo. Rais hakufurahishwa na hilo. Sasa tunahitaji kusonga mbele na kufahamu nini kitakachofuata.”
Mkutano huo unakuja wakati viongozi wa nchi za kiarabu wakifanya mkutano wa kilele kuonyesha uungaji mkono kwa Qatar. Waziri mkuu wa Qatari aliitaka jumuiya ya kimataifa kuacha kutumia “undumilakuwili” na kuiadhibu Israel.
Nchi hiyo ya Ghuba ni makazi ya kambi kubwa ya jeshi la anga la Marekani na imekuwa na jukumu muhimu katika kufanikisha juhudi za kidiplomasia kumaliza vita huko Gaza, ikisimama kama mpatanishi wa mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Hamas na Israel.
Siku ya Jumapili, Netanyahu aliwaambia waandishi wa habari kwamba uhusiano wa Marekani na Israel ni “imara kama mawe katika Ukuta wa Magharibi” wakati yeye na Rubio walipofanya ziara fupi kwenye eneo takatifu katika Jiji la Kale la Jerusalem.
Katika ziara hiyo – ambayo pia ilikuwa na balozi wa Marekani nchini Israel Mike Huckabee – Rubio aliandika ujumbe na kuuweka ukutani. Viongozi hao wawili walipuuza maswali ya wanahabari yanayolenga kuhoji shambulizi la Israel nchini Qatar.
Ajenda nyingine inayotarajiwa kujadiliwa na wawili hao ni mipango ya jeshi la Israel kuuteka mji wa Gaza na kuendelea kwa Israel kupanua makaazi ya walowezi katika Ukingo wa Magharibi.
Mkutano huo unakuja kabla ya mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wiki ijayo, ambapo baadhi ya washirika wakuu wa Marekani – ikiwa ni pamoja na Uingereza, Ufaransa, Kanada, Australia na Ubelgiji – wanatarajiwa kulitambua taifa la Palestina.
“Chuki kati ya Zelensky na Putin haielezeki” – Trump

Rais Donald Trump anadai chuki kati ya Vladimir Putin wa Urusi na Volodymyr Zelensky wa Ukraine “haiwezi kuelezeka” huku rais huyo wa Marekani akiendeleza juhudi za kupatikana kwa amani katika nchi hizo mbili.
Trump kwa mara nyingine alisema kwamba kumaliza vita huko Ukraine kumegeuka kuwa suala gumu kuliko alivyotarajia.
“Nilisitisha vita saba – nilidhani hii itakuwa rahisi kwangu, lakini imegeuka kuwa vigumu sana,” aliwaambia waandishi wa habari siku ya Jumatatu.
“Chuki kati ya Zelensky na Putin haielezeki … wanachukia sana, bado kidogo tu wasizungumziane.”
Alipoulizwa ikiwa anaamini Putin na Zelensky watajadiliana, Trump alisema: “Sijui. Nafikiri itabidi nifanye mazungumzo nao.”
Trump aliongeza kuwa hilo linaweza kutokea “hivi karibuni.”
Alipoulizwa ikiwa mkutano wa tatu unaweza kufuata, Trump alisema jinsi itakavyokuwa haina maana: “Kutakuwa na mazungumzo – ikiwa mutayaita mkutano wa kilele au mkutano tu, haijalishi. Lakini labda itabidi nihusike. Wanachukiana sana kiasi kwamba ni vigumu wao wenyewe kuzungumza.”
Tume ya Uchaguzi Tanzania yamuondoa Mpina katika majina ya wagombea wa Urais

Mgombea urais kwa tiketi ya ACT Wazalendo Luhaga Joelson Mpina amekutana na kizingiti kingine baada ya Tume ya Uchaguzi kuondoa jina lake kwenye orodha ya wagombea wa kiti cha urais.
Uamuzi huo wa Tume umetokana na pingamizi lililowekwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Hamza Said Johari dhidi ya Mpina.
Mpina ameondolewa kwenye orodha ya wagombea siku nne tu baada ya kushinda kesi katika Mahakama Kuu Masjala Kuu ya Dodoma alipokuwa akipinga uamuzi wa awali wa Tume wa kumzuia kurudisha fomu ya kuteuliwa kugombea nafasi ya Urais.
Kwa mujibu wa taarifa ya ACT Wazalendo, pingamizi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali lilidai kwamba Mpina hakuwa na sifa ya kuwa Mgombea wa Urais kufuatia uamuzi wa awali Msajili wa Vyama Vya Siasa.
Katika taarifa yake kwa umma, ACT Wazalendo kilikitupia lawama Chama Cha Mapinduzi (CCM) juu ya mapingamizi yaliyowekwa dhidi ya mgombea wake Mpina kikidai kwamba mapingamizi hayo hayakuwa na ukweli wala msingi wowote.
Haijafahamika bado ikiwa ACT Wazalendo watarudi mahakamani kupinga tena pingamizi hili jipya la Tume ya Uchaguzi.
Israel yazidisha mashambulizi mjini Gaza huku Rubio ikiwasili

Vikosi vya Israel vimeharibu takriban majengo 30 ya makazi katika mji wa Gaza na kuwalazimisha maelfu ya watu kuondoka makwao, maafisa wa Palestina wamesema, wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alipowasili Jumapili kujadili mustakabali wa mzozo huo.
Israel imesema inapanga kuuteka mji huo, ambapo takriban Wapalestina milioni moja wamekuwa wakijihifadhi, ikiwa ni sehemu ya lengo lake lililotangazwa la kulitokomeza kundi la wanamgambo wa Hamas, na kuzidisha mashambulizi dhidi ya kile ilichokiita ngome ya mwisho ya kundi la wapiganaji wa Palestina.
Uongozi wa kisiasa wa Hamas, ambao umekuwa na mazungumzo ya mara kwa mara juu ya uwezekano wa kusitisha mapigano na kuachiliwa kwa mateka, ulilengwa na Israel katika shambulio la anga huko Doha siku ya Jumanne katika shambulio ambalo lilishutumiwa na watu wengi.
Qatar itakuwa mwenyeji wa mkutano wa dharura wa kilele wa viongozi wa Kiarabu na Kiislamu siku ya Jumatatu kujadili hatua zinazofuata.
Rubio alisema Washington ilitaka kuzungumza kuhusu jinsi ya kuwakomboa mateka 48 ambao bado wanashikiliwa na Hamas katika Ukanda wa Gaza na kujenga upya ukanda wa pwani. Ni 20 pekee wanaoaminika kuwa hai.
“Kilichotokea kimetokea,” alisema. “Tutakutana nao (uongozi wa Israel). Tutazungumza kuhusu hatma ya siku zijazo,” Rubio alisema kabla ya kuelekea Israel ambako atakaa hadi Jumanne.
Mtanzania ashinda dhahabu ya kwanza katika mashindano ya dunia Japan

Baada ya mbio za kilomita 42.195 katika mazingira magumu, mbio za marathoni za Riadha za Dunia za 2025 kwa wanaume ziliamuliwa kwa tofauti ndogo
Katika umaliziaji uliovutia wengi ndani ya Uwanja wa Taifa wa Japan mjini Tokyo Jumatatu Septemba 15, Alphonce Simbu wa Tanzania alivuka mstari wa kumalizia mbele ya Mjerumani Amanal Petros na kushinda taji la dunia kwa saa 2:09:48.
Dhahabu ya dunia ya Simbu ni ya kwanza kwa mwanariadha wa Tanzania kuwahi kushinda katika riadha na uwanjani.
Pia ushindani huo ulikuwa wa karibu mno ikiwa tofauti ya sekunde 0.03 katika mbio za marathon kwenye michuano ya dunia.
“Nimeweka historia leo, ikiwa ni medali ya kwanza ya dhahabu ya Tanzania katika mashindano ya dunia,” Simbu alisema baada ya ushindi wake. “Nakumbuka mwaka 2017, kwenye mashindano ya dunia ya London, nilishinda shaba.
Kisha nilikimbia mara nyingi lakini sikupata medali yoyote, hivyo hatimaye ni hapa. Nilipofika hapa, nilijiambia kuwa sitakata tamaa. Nilibaki tu na kundi; ilinisaidia, na mashindano yalimalizika vizuri sana.
Angalia tu kumaliza na mguu.” Petros alimaliza mbio hizo kwa muda sawa na Simbu na, ingawa alijilaza sakafuni huku akiwa amezingirwa na mkanda wa kumalizia, atahitaji kuridhika na medali ya fedha.
Muigizaji nyota Owen Cooper aweka historia katika tuzo za Emmy

Muigizaji wa Uingereza Owen Cooper amekuwa kijana mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kushinda Tuzo ya Emmy ya muigizaji bora msaidizi.
Cooper, 15, alitajwa kutokana na uhusika wake kama mvulana wa shule anayetuhumiwa kumuua mwanafunzi mwenzake.
Filamu anayoshiriki ya mfululizo wa sehemu nne pia imechukua tuzo la filamu bora, pamoja na uelekezi na uandishi bora, na tuzo za uigizaji za Stephen Graham na Erin Doherty.
Katika hotuba yake ya kukubalika tuzo yake, Cooper alisema: “Kusimama hapa ni jambo jema sana…
“Nilipoanza masomo haya ya maigizo miaka kadhaa nyuma, sikutarajia hata kutambulika Marekani, licha ya hapa.”
Cooper, ambaye aliigiza kama kijana Jamie Miller, alisema: “Nadhani usiku wa leo unathibitisha ikiwa unasikiliza, na unazingatia na kujituma, unaweza kufikia chochote maishani.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.