Msimamo wa Donald Trump juu ya adhabu ya kifo

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Rais Donald Trump hapo jana alitoa wito kwa mshukiwa wa mauaji ya Charlie Kirk Tyler Robinson kuhukumiwa kifo.

Trump amekuwa akionyesha kupendelea adhabu ya kifo kwa muda mrefu na aliondoa kusitishwa kwa hukumu hiyo na serikali kupitia agizo la rais siku ya kwanza ya utawala wake wa pili mnamo mwezi Januari.

Idadi kubwa ya hukumu za kifo nchini Marekani hutekelezwa katika ngazi ya majimbo, huku 27, jeshi na serikali kuu zikiwa bado zinatekeleza adhabu ya kifo kama chaguo linalotekelezwa kisheria.

Ingawa hakuna hukumu ya kifo ya serikali iliyotekelezwa tangu Trump arudi ofisini, alipitisha msururu wa hukumu 13 za kifo katika miezi ya muhula wake wa kwanza mwishoni mwa 2020 na Januari 2021.

Hukumu hizo za kifo zilimfanya Trump kuwa mkuu wa nchi aliyewahi kupitisha nyingi zaidi ya karne moja.

Utekelezaji wa mwisho ulifanyika siku tano tu kabla ya kuondoka madarakani mnamo Januari 2021.

Ujumbe mpya wa NATO waimarisha eneo la mashariki baada ya uvamizi wa ndege za Urusi

.

Nchi zaidi za Nato zitahamisha wanajeshi wao na ndege za kivita kuelekea mashariki baada ya Poland kuishutumu Urusi kwa uvamizi wa ndege zisizo na rubani siku ya Jumatano.

Denmark, Ufaransa na Ujerumani zimejiunga na misheni mpya ya kuimarisha upande wa mashariki wa muungano wa kijeshi. Washirika wengine wa Nato wanatarajiwa kushiriki baadaye.

Hatua hii inawadia baada ya Kremlin kusema siku ya Ijumaa kwamba mazungumzo ya amani na Kyiv yalikuwa “yamesitishwa”, msemaji Dmitry Peskov akisema: “Huwezi kupuuza yanayotokea na kutarajia kwamba mchakato wa mazungumzo utakuwa na matokeo ya haraka.”

Mvutano wa kisiasa umekuwa mkubwa kote barani Ulaya baada ya Poland kusema ndege 19 zisizo na rubani za Urusi zilipitia anga yake siku ya Jumatano.

Baadhi yao zilidunguliwa, huku zingine zikianguka kwenye mashamba na hata nyumba moja mashariki mwa Poland.

Mahakama ya Colombia yasema Meta alikosea kwa kufunga akaunti ya Instagram ya nyota wa ponografia

.

Mahakama ya juu zaidi nchini Colombia imetoa uamuzi na kusema kuwa Meta ilikiuka haki ya uhuru wa kujieleza wa nyota wa ponografia ilipofuta akaunti yake ya Instagram.

Mahakama ya Kikatiba ya taifa la Amerika Kusini ilisema Ijumaa kwamba Meta iliondoa akaunti ya Esperanza Gómez “bila sababu ya msingi” na bila kufanya kama hivyo kwa akaunti zingine zenye maudhui sawa na yake.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 45, ambaye akaunti yake ilikuwa na wafuasi zaidi ya milioni tano, ni mmoja wa waigizaji maarufu wa maudhui ya watu wazima nchini Colombia.

Meta alisema katika kesi hiyo kwamba alikuwa amekiuka sheria zake kuhusu uchi. Kampuni hiyo, ambayo pia inamiliki Facebook na WhatsApp, haikujibu mara moja uamuzi huo.

Othman Masoud wa ACT Wazalendo aahidi wapiga kura mabadiliko

.

Mgombea urais wa Zanzibar kupitia ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman, amesema endapo atachaguliwa kuwa Rais, atahakikisha mipango ya maendeleo kwa wafanyakazi wa serikali na walimu inatekelezwa mara moja, huku akisisitiza usawa na heshima kwa kila mtumishi wa Zanzibar.

Othman alitoa kauli hiyo wakati akihutubiakwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mkuu katika viwanja vya Tibirinzi, Chake Chake, Pemba na kusisitiza kuwa mabadiliko hayana budi kuanza sasa.

Alisema moja ya hatua za haraka atakazochukua ni kuhakikisha askari wote wa vikosi vya Usalama wa Mapinduzi Zanzibar (SMZ) wanapata mshahara usiopungua milioni moja, hatua ambayo itaimarisha familia zao na kuongeza morali ya utumishi wa taifa.

ACT Wazalendo yalikataa gari la INEC Tanzania, yazindua kampeni Zanzibar

.

Chama cha ACT Wazalendo kimelikataa gari jipya lilitolewa na kwa mgombea wake wa urais, Luhaga Mpina na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (INEC)

Uamuzi huo wa kulikataa gari umetangazwa na Mwanasheria Mkuu wa wa chama hicho, Omar Shaban mara baada ya Mpina kuteuliwa na INEC kuwa mgombea wa urais wa Tanzania na Fatma Fereji kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.

Tangazo la kupatiwa gari jipya lilitolewa na Mwenyekiti wa INEC jaji mstaafu Jacobs Mwambegele ambaye alisema, “Pamoja na kuwapongeza kwa uteuzi wenu, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi inakukabidhi mgombe wa kiti cha rais gari moja jipya aina ya Land Cruiser GX-VXR kwa ajili ya kampeni. Hivyo namuelekeza Mkurugenzi wa Uchaguzi wakati anawasindikiza, akakukabidhi gari hilo pamoja na dereva atakayekuhudumia muda wote wa kampeni asante tunawakia kampeni zenye mafanikio”.

Mara tu baada ya jaji Mwambegele kumaliza kutoa maelezo ya gari, papo hapo akainuka Mwanasheria Mkuu wa ACT, Omar Shaban akasema: Kwanza tunashukuru sana kwa ukarimu ambao tumeelezwa kuhusu kumkabidhi mgombea gari Pamoja na walinzi.

Nimeagizwa na kamati ya uongizu wa chama kushukuru kuhusu jambo hili, lakini pamoja na hayo chama kimenielekeza ni-communicate kuwa kwenye rasilimali ya gari tunashukuru tuko vizuri, tutaomba lisaidie kwa matumizi mengine.

Kwa uamuzi huo ACT Wazalendo kinakuwa chama cha kwanza cha siasa na cha pekee miongoni mwa vyama 18 vinavyoshiriki uchaguzi mkuu wa Tanzania 2025 kulikataa gari jipya la INEC. Wagombea wengine 17 akiwemo Samia Suluhu Hassan wa CCM walikabidhiwa magari mapya Agosti 27, 2025 ambayo ilikuwa siku ya uteuzi wa wagombea wa nafasi ya urais.

Siku hiyo Mpina na mgombea mwenza Fereji walizuiwa kuingia ofisi za INEC kukabidhi fomu, hivyo ACT na Mpina waliamua kwenda Mahakama Kuu kuupinga uamuzi kwa kumuengua mgombea kwa sababu ya kukosa vigezo.

Alhamisi Septemba 11, jopo la majaji watatu; Abdi Kagomba (kiongozi wa jopo), Evaristo Longopa, na John Kahyoza lilkubaliana na hoja za msingi za walalamikaji dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na INEC, hususan kukiukwa kwa Katiba ya Tanzania, inayotoa uhuru kamili kwa INEC na kuzuiwa kupokea maelekezo kutoka kwa mtu au taasisi yoyote na pia walalamikaji kutopewa fursa ya kusikilizwa. Hivyo jopo hilo likawapa ushindi walalamikaji.

Wazindua kapeni za urais Zanzibar

.

Wakati huohuo, maelfu ya wanachama na wafuasi wa chama cha ACT Wazalendo wamejitokeza kwa wingi katika uwanja wa Tibirinzi, Chake Chake, Pemba kushiriki uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mkuu. Mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama hicho, Othman Masoud Othman, ndiye mgeni rasmi katika uzinduzi huo. Viongozi mbalimbali ACT Wazalendo pia wamehudhuria, akiwemo aliyekuwa kiongozi mkuu, Zitto Kabwe.

Zitto ameiambia hadhara ya uzinduzi wa kampeni kwamba fursa pekee iliyobakia kwa Zanzibar kurudisha heshima na mamlaka yake ni kumchagua Othman Masoud Othman kuwa Rais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Amesema amemfahamu Othman Masoud kwa muda mrefu na anamtambua kama kiongozi mwenye msimamo wa kweli na aliye tayari kupigania maslahi ya Zanzibar bila kuyumba.

Alikumbusha kuwa wakati akiwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman hakusita kupambana hadharani akitetea mamlaka ya Zanzibar hata pale alipofukuzwa kazi, lakini alibaki imara na thabiti.

.

Kwa mujibu wa Zitto, msimamo huo ni ushahidi tosha kwamba Othman ni lulu ya Zanzibar, kiongozi shupavu anayeweza kuongoza wananchi kwa ujasiri na hekima.

Aidha, Zitto aliwakumbusha wananchi dhamira njema ya marehemu Maalim Seif Sharif Hamad, akieleza kuwa njia aliyoiacha Maalim ndiyo tunu ya Zanzibar mpya na Othman ndiye mwendelezo wa ndoto hiyo.

Zitto aliongeza kuwa hali ya maisha ya wananchi imekuwa ngumu, na kwamba suluhisho pekee ni kumpa kura Othman Masoud. Alisisitiza kuwa chini ya uongozi wa Othman, Zanzibar itarudisha heshima yake, itashika nafasi ya uchumi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, na wananchi watanufaika moja kwa moja na rasilimali zao.

Watu wafa maji baada ya boti kuzama DR Congo

.

Karibu watu 200 wamekufa maji huku wengine wakiwa hawajulikani walipo kufuatia ajali mbili tofauti za mashua katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kaskazini Magharibi mwa Congo.

Kikundi cha asasi za kiraia kimelaumu serikali na kudai idadi ya walioaga dunia ni kubwa.

Timu za uokoaji bado zinatafuta manusura kufuatia ajali mbaya katika mkoa wa equateur wiki hii.

Karibu watu 150 bado hawajapatikana kufuatia moto kwenye mashua Alhamisi usiku kabla ya kuzama kwenye mto wa Congo.

Siku iliyopita ajali tofauti iliua abiria zaidi ya 80, haswa wanafunzi. Ripoti zinasema chombo hicho kilikuwa kimebeba abiria wengi kupita kiasi.

Rubani wa Nigeria athibitishwa amekunywa kileo baada ya ndege kuacha njia

.

Rubani na rubani mwenza wamepimwa na kuthibitishwa kuwa wamekunya pombe baada ya ndege waliyokuwa wakiendesha kuacha njia ilipokuwa ikitua nchini Nigeria.

Ofisi ya Uchunguzi wa Usalama wa Nigeria (NSIB) iliwachunguza wawili hao baada ya kutokea kwa ajali mwezi Julai, katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Port Harcourt. Vile vile, mfanyakazi wa ndege hiyo alipimwa na kukutwa ametumia bangi.

Watu wote 103 waliokuwa kwenye ndege hiyo aina ya Boeing 737 wakati kisa hicho kinatokea hawakudhurika.

Kampuni ya Air Peace, iliyoendesha ndege hiyo, ilisema rubani huyo mwenye umri wa miaka 64 amefutwa kazi kwa kushindwa kuzingatia kanuni za usalama, wakati rubani msaidizi amerejea kwenye jukumu lake.

Quad yatoa wito wa usitishaji mapigano huko Sudan

.

Marekani, Misri, Saudi Arabia na UAE kwa pamoja wametoa wito wa kusitishwa mapigano kwa miezi tatu huko Sudan hatua ambayo itakuwa mwanzo wa usitishaji mapigano wa kudumu na kukaribisha kipindi cha mpito cha miezi 9 hadi kupatikana kwa serikali ya raia.

Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka Kikundi cha Mataifa kinachojulikana kama Quad walikutana huko Washington na kukubaliana kutumia ushawishi wao kusaidia kutafuta makubaliano ya usitishaji mapigano na pande husika – vikosi vya jeshi la Sudan na Rapid Support Forces.

Mawaziri hao hata hivyo walisema hakuna upande wowote unaozozana utakaosimamia kipindi cha mpito hadi kupatikana kwa serikali ya kiraia.

Quad pia ilisisitiza hitaji la Sudan kusalia na umoja na kuwa msaada wa jeshi kutoka nchi za nje ukomeshwe kwa pande zote mbili.

UAE, mwanachama wa Quad, ameshtumiwa kwa kuunga mkono RSF, shutuma ambazo imekanusha mara kwa mara.

Jeshi la Sudan na RSF wameanzisha serikali mbadala zenye mawaziri wakuu na makatibu katika wiki za hivi karibuni.

Kundi hilo la mawaziri lilisema kwamba hali ilivyo sasa hivi “inasababisha mateso yasiyokubalika” na kuongeza kuwa uingiliaji wa kijeshi hakuwezi kuleta suluhu.

Vita huko Sudan viliibuka mnamo Aprili 2023 kati ya jeshi la nchi hiyo na kikosi cha wanajeshi wanaotembea kwa miguu cha RSF.

Mzozo huo umesababisha matatizo makubwa ya kibinadamu ulimwenguni, makumi ya maelfu wakiuawa huku mamilioni wakilazimika kuhama makazi yao.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment