Makamu wa rais wa Sudan Kusini ashtakiwa kwa mauaji na uhaini

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudan Kusini Riek Machar amefunguliwa mashtaka ya mauaji, uhaini na uhalifu dhidi ya binadamu hatua ambayo baadhi ya watu wanahofia inaweza kuzusha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Makamu wa rais wa Sudan Kusini ashtakiwa kwa mauaji na uhaini

g
Maelezo ya picha,Riek Machar amekuwa chini ya kizuizi cha nyumbani tangu Machi

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudan Kusini Riek Machar amefunguliwa mashtaka ya mauaji, uhaini na uhalifu dhidi ya binadamu hatua ambayo baadhi ya watu wanahofia inaweza kuzusha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Waziri wa Sheria Joseph Geng Akech alisema mashtaka dhidi ya Machar yanahusiana na shambulio la mwezi Machi na wanamgambo wanaodaiwa kuhusishwa na makamu wa rais.

Barabara zinazoelekea kwenye nyumba yake katika mji mkuu, Juba, zimefungwa na vifaru na wanajeshi.

g
Maelezo ya picha,Kumekuwa na uhasama kati ya wa muda mrefu Rais Salva Kiir ( kulia) na Riek Mchar

Vikosi vinavyomtii Machar vilipigana vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka mitano dhidi ya vile vinavyomuunga mkono Rais Salva Kiir hadi makubaliano ya amani ya 2018 yanayomaliza mapigano katika nchi hiyo mpya zaidi duniani.

Bwana Machar amekuwa chini ya kifungo cha nyumbani tangu mwezi Machi, huku Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na nchi jirani zikitoa wito wa utulivu.

Makubaliano ya amani ya mwaka 2018 yalimaliza mzozo uliosababisha vifo vya takriban watu 400,000, hata hivyo uhusiano kati ya Machar na Kiir umezidi kuwa mbaya huku kukiwa na mivutano ya kikabila na ghasia za hapa na pale.

Wengine saba wameshtakiwa pamoja na Machar, akiwemo Waziri wa Petroli Puot Kang Chol na Naibu Mkuu wa Majeshi Lt Jenerali Gabriel Duop Lam, Waziri wa Sheria Joseph Geng Akech alisema katika taarifa.

Wote ni washirika wa Machar ambao walikamatwa kwa wakati mmoja na yeye na pia wamekuwa kizuizini tangu wakati huo. Washukiwa wengine 13 bado hawajakamatwa, waziri alisema.

Burkina Faso kutoa viza bila malipo kwa raia wa Afrika

h

Burkina Faso inasema imeanzisha mfumo wa viza bila malipo kwa raia wa Afrika, kwa nia ya kuwezesha usafirishaji wa watu na bidhaa ndani ya nchi.

Uamuzi huo ulichukuliwa Alhamisi, wakati wa mkutano wa baraza la mawaziri ulioongozwa na kiongozi wa kijeshi Kapteni Ibrahim Traoré

“Kuanzia sasa, raia yeyote kutoka nchi ya Kiafrika anayetaka kwenda Burkina Faso hatalipa kiasi chochote cha kulipia ada ya visa,” alisema Mahamadou Sana, Waziri wa usalama.

Kulingana na huduma ya habari ya serikali, kufuta ada ya viza kwa raia wa bara hilo kunaonyesha kushikamana kwa Burkina Faso na maadili ya Kiafrika (Pan-Africanist), na kukuza ushirikiano wa kikanda.

“Mfumo huu wa viza bila malipo kwa raia wa Kiafrika pia utasaidia kukuza utalii na utamaduni wa Burkinafaso, na kuboresha taswira ya Burkina Faso nje ya nchi,” taarifa kutoka huduma ya serikali iliongeza.

Ingawa Waafrika hawatakiwi tena kulipa ada ili kuingia katika taifa hilo la Afrika Magharibi, bado wanalazimika kutuma maombi ya mtandaoni kabla ya kusafiri. Ombi lao litapitiwa na kuidhinishwa, Waziri wa usalama alifafanua.

Burkina Faso, taifa la Sahel ambalo kwa sasa linakabiliwa na vitisho vya usalama kutoka kwa waasi, linaongozwa na mwanajeshi mchanga ambaye amesifiwa kwa msimamo wake wa uafrika.

Kapteni Traoré alichukua madaraka katika mapinduzi ya 2022 lakini tangu wakati huo ameshindwa kutimiza ahadi yake ya kurejesha usalama.

Burkina Faso sasa ni miongoni mwa nchi kama vile Ghana, Rwanda, na Kenya, ambazo hivi majuzi zilipunguza mahitaji ya kusafiri kwa wageni wa Kiafrika.

Bado haijulikani ikiwa hatua hii itasaidia kuboresha taswira ya nchi huku kukiwa na ukosoaji unaoongezeka dhidi ya jeshi.

Bolsonaro ahukumiwa kifungo cha miaka 27 jela kwa kupanga njama ya mapinduzi ya Brazil

g
Maelezo ya picha,Jair Bolsonaro alipatikana na hatia ya mashtaka matano

Rais wa zamani wa Brazil, Jair Bolsonaro, amehukumiwa kifungo cha miaka 27 na miezi mitatu jela baada ya kupatikana na hatia ya kupanga mapinduzi ya kijeshi.

Jopo la majaji watano wa Mahakama ya juu lilitoa hukumu hiyo saa chache baada ya kumpata na hatia kiongozi huyo wa zamani.

Walisema ana hatia ya kuongoza njama iliyolenga kumuweka madarakani baada ya kushindwa katika uchaguzi wa 2022 na mpinzani wake wa mrengo wa kushoto, Luiz Inácio Lula da Silva.

Jopo la Mahakama ya Juu pia lilimzuia kuwania wadhifa wa umma hadi 2033.

Bolsonaro, ambaye aliwekwa chini ya kizuizi cha nyumbani baada ya kutajwa kuwa ana hatari ya kukimbia, hakuhudhuria awamu hii ya mwisho ya kesi ana kwa ana.

Lakini siku za nyuma alisema ilibuniwa kumzuia kugombea katika uchaguzi wa urais wa 2026 – ingawa tayari alikuwa amezuiliwa kuongoza ofisi ya umma kwa mashtaka tofauti. Pia ameiita kesi hiyo “uonevu”.

Maneno yake hapo awali yameungwa mkono na Rais wa Merika, Donald Trump, ambaye aliweka ushuru wa 50% kwa bidhaa za Brazil, kama kulipiza kisasi kwa mashtaka dhidi ya Bolsonaro.

Polisi Marekani yatoa video rasmi inayomuonyesha mshukiwa akitoroka eneo la tukio alikopigwa risasi Charlie Kirk

Maelezo ya video,Tazama : Video mpya polisi akielezea wakati mtu anayeshukiwa kumpiga risasi Kirk akitoroka kutoka eneo la tukio

Maafisa usalama wametoa video mpya ya mshukiwa, ambapo anaonekana akikimbia kwenye paa la jengo ambalo risasi mbaya ilifyatuliwa na kukimbia eneo la tukio.

Mshukiwa huyo alikuwa amevalia miwani ya jua, viatu vya raba na t-shirt nyeusi “ya kipekee” yenye bendera ya Marekani na tai.

Kamishna wa Idara ya Usalama wa Umma wa Utah Beau Mason alionyesha picha “zilizoboreshwa” za mshukiwa , na akasema vidokezo vya umma “vinatupa mwongozo wetu”

Polisi imesema imepokea zaidi ya vidokezo 7,000 hadi sasa , huku Gavana wa Utah Spencer Cox akisema ni idadi kubwa zaidi ambavyo FBI imepokea tangu shambulio la bomu la Boston Marathon mnamo 2013.

Akizungumza na kipindi cha BBC Newsday mkurugenzi msaidizi mstaafu wa FBI, Chris Piehota, amesema kuna uwezekano FBI bado iko katika hatua ya kukusanya na kuchambua data kutoka kwa upigaji risasi, ikiwa ni pamoja na picha kutoka kwa vifaa vya kibinafsi, picha za uchunguzi na klipu za sauti.

Alisema “ana imani” kwamba watamkamata mpiga risasi.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment