Qatar yasema msako unaendelea katika eneo la mashambulizi ya Israel yaliyoyowalenga viongozi wa Hamas

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mamlaka ya Qatar inasema bado inawasaka watu wawili waliotoweka na kuyatambua masalia ya miili ya binadamu baada ya shambulio la Israel lililowalenga viongozi wakuu wa Hamas mjini Doha siku ya Jumanne.

Mamlaka ya Qatar inasema bado inawasaka watu wawili waliotoweka na kuyatambua mabaki ya binadamu baada ya shambulio la Israel kuwalenga viongozi wakuu wa Hamas mjini Doha siku ya Jumanne.

Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kuwa kuna wasiwasi katika duru za kijeshi za Israel kwamba shambulio hilo lenye utata mkubwa halikufanikiwa.

Wizara ya mambo ya ndani ya Qatar imeitambua miili ya wanachama watatu kati ya watano wa ngazi ya chini wa Hamas ambao kundi lenye silaha la Palestina lilisema waliuawa pamoja na afisa wa usalama wa Qatar.

Hamas imedai jaribio la kuua timu yake ya mazungumzo lilishindikana. Katika mahojiano na CNN, waziri mkuu wa Qatar hakufichua hatma ya mpatanishi mkuu wa Hamas Khalil al-Hayya.

“Hadi sasa… hakuna tamko rasmi,” Sheikh Mohammed bin Abdul Rahman Al Thani alisema Jumatano jioni.

Pia alisema hatua ya Israel ni sawa na “ugaidi wa serikali” na kwamba anatumai washirika wa likanda wa Qatar watakubali “jibu la pamoja”.

Ghana yakubali kuwapokea raia wa Afrika Magharibi waliofukuzwa kutoka Marekani

g
Maelezo ya picha,Rais wa Ghana John Mahama

Rais wa Ghana John Mahama amethibitisha kuwa nchi hiyo imekubali kuwapokea raia wa Afrika Magharibi waliofukuzwa kutoka Marekani.

Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Accra, Rais Mahama alifichua kuwa watu 14 waliofukuzwa, wengi wao wakiwa Wanigeria na mmoja wa Gambia, tayari wamewasili Ghana chini ya makubaliano ya nchi mbili.

Rais Mahama alieleza kuwa Marekani iliwasiliana na Ghana kukubali raia watatu kuondolewa Marekani, na Ghana ilikubali kuwakubali raia wa Afrika Magharibi, akitoa mfano wa Itifaki ya ECOWAS kuhusu uhuru wa harakati huru. Itifaki hiyo inaruhusu raia wa nchi wanachama kuingia na kuishi katika nchi nyingine za Afrika Magharibi bila viza kwa hadi siku 90.

“Hatuna shida kuwakubali,” Rais Mahama alisema, akiongeza kuwa Ghana iliwezesha kurejeshwa kwa rais wa Nigeria waliofukuzwa nchini mwao kwa basi, wakati raia wa Gambia akisaidiwa na mamlaka ya Ghana na ubalozi wa Gambia nchini Ghana.

Hii ni sehemu ya juhudi za utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump kuwafukuza mamilioni ya wahamiaji ambao wako Marekani kinyume cha sheria, huku baadhi ya nchi za Kiafrika zikiwa tayari zinapokea wahamiaji waliofukuzwa. Rwanda, Sudan Kusini, na Eswatini zimekubali kuwapokea raia waliofukuzwa kutoka Marekani.

Trump alaani mauji ya mshawishi wa kisiasa na mshirika wake aliyepigwa risasi

g
Maelezo ya picha,Charlie Kirk alipigwa kupigwa risasi alipokuwa akizungumza katika hafla katika Chuo Kikuu cha Utah Valley.

Rais wa Marekani amelaani kifo cha Charlie Kirk Kirk aliyekuwa alikuwa mmoja wa wanaharakati wahafidhina (Conservative) mashuhuri na mwanahabari nchini Marekani na mshirika wa kutumainiwa wa Rais Donald Trump.

Ameyataja mauaji ya Charlie Kirk ‘wakati wa giza kwa Marekani’ huku msako mkali ukiendelea kuwapata wahusika wa shambulio hilo, lililowashutua Wamarekani.

Charlie Kirk , 31, aliuawa kwa kupigwa risasi alipokuwa akizungumza katika hafla katika Chuo Kikuu cha Utah Valley.

Kirk alipigwa risasi moja shingoni, video iliyothibitishwa na kitengo cha uhakiki wa habari cha BBC -BBC Verify, imeonyesha.

Hakuna mtu mwingine aliyepigwa risasi wakati wa tukio hilo. Mshambuliaji bado hajakamatwa.

Mke na watoto wa Kirk walikuwepo wakati wa ufyatuaji risasi, kulingana na Seneta wa Oklahoma Markwayne Mullins

Bado hakuna sababu inayojulikana ya upigaji risasi huo

Mnamo 2012, akiwa na umri wa miaka 18, alianzisha shirika la Turning Point USA, shirika la wanafunzi ambalo linalenga kueneza maadili ya kihafidhina katika vyuo vya Marekani.

Mitandao yake ya kijamii na podikasti ya kila siku iliyojulikana mara nyingi alikuwa akijadiliana na wanafunzi kuhusu masuala kama vile utambulisho wa watu waliobadili jinsia, mabadiliko ya hali ya hewa, imani na maadili ya familia.

Kirk alikuwa ameoa na alikuwa na watoto wawili wadogo, ambao walikuwa naye wakati wa tukio la ufyatuaji risasi.

Mauji yake pia yamelaaniwa na viongozi mbali mbali wa kisiasa wa Marekani na nje ya nchi, walioyataji kama yasiyokubalika na kutoa wito wahusika waadhibiwe ili kuyakomesha.

 Ethiopia yasherehekea mwaka mpya

g
Maelezo ya picha,Barabara hupambwa kwa taa za kuvutia

Wakati majira ya baridi kali yanapoisha, hali ya hewa ya baridi inafifia, nuru huanza kuangaza, na dunia kupambwa na kijani kibichi na maua, Waethiopia waanza mwaka wao mpya.

Sherehe hii hupambwa kwa maua ya Adai, ambayo huashiria mwisho wa mwaka wa awali na mwanzo wa mpya.

Mwewe, ambao huashiria mwisho wa majira ya baridi na mwanzo wa enzi mpya, pia huanza kuonekana akiwa na manyoya yake mapya.

Waethiopia wanasherehekea mwaka wao mpya mnamo Septemba 1, wakikamilisha miezi 13 inayoufanya mwaka wao kuwa wa kipekee tofauti na maeneo mengine duniani ambako mwaka huwa na miezi 12.

Muda nao uhesabiwa tofauti

Muda unahesabiwa tofauti -ambapo siku ikiwa imegawanywa sehemu mbili za masaa 12 kuanzia 06:00, ambayo inafanya mchana na usiku wa manane saa sita kwa wakati wa Ethiopia.

Kwahiyo ukipanga kikao na mtu aliyeko Addis Ababa saa nne asubihi kwaajili ya kahawa-usishangae ukamuona huyo mtu akitokea saa sita.

Hizi ni baadhi ya picha za sherehe za Mwaka mpya wa Ethiopia:

g
Maelezo ya picha,Masoko hufurika wanyama wanyama wanaochinjwa kwa ajili ya sherehe za mwaka mpya
g
Maelezo ya picha,Kuku pia ni kitoweo kinachopendwa na Waethiopia katika sherehe za mwaka mpya
g
g
h
Maelezo ya picha,Maua haya huashiria kipindi cha Mwaka mpya
h
g
Maelezo ya picha,Waromania huvaa mavazi ya ngozi ya dubu kuadhimisha Mwaka Mpya
g

Kwa maelezo zaidi ya taarifa hii unaweza kusoma:

Arusha: Mwendesha mashtaka aomba Kabuga arejeshwe Rwanda

Kabuga
Maelezo ya picha,Félicien Kabuga akiwa katika mahakama ya The Hague, Uholanzi, mwaka jana

Mwendesha mashitaka wa kitengo cha Mahakama ya kimataifa ya mauaji ya kimbari ya Rwanda (ICTR) kilichosalia kusikiliza kesi zilizoachwa na Mahakama hiyo ya Arusha amekitaka kitengo hicho kufanya utafiti wa kuachiwa kwa muda kwa Félicien Kabuga na kuhamishiwa Rwanda, nchi alikozaliwa ambayo “ndio pekee imeonyesha nia ya kumpokea”, kwa mujibu wa waraka kutoka katika kitengo hicho.

Kwa sasa Kabuga anazuiliwa katika gereza la The Hague, Uholanzi, baada ya chumba cha taasisi inayofanya kazi huko mnamo mwezi Septemba, 2024 kuamua kusitisha kwa muda usiojulikana kesi ya Kabuga mwenye umri wa miaka 90 kwa misingi ya afya, na kwamba ataachiliwa kwa dhamana.

Kabuga alishtakiwa kwa uhalifu ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wa kifedha kwa mauaji ya kimbari ya 1994 nchini Rwanda, mashtaka aliyoyaita “uongo”.

Jumanne mjini Arusha, Tanzania, jopo la majaji watatu; Iain Bonomy, Mustapha El Baaj na Margaret M. deGuzman na ripota Bw. Abubacarr M. Tambadou msajiliwa mahakama walijadili kuhusu kuachiliwa kwa muda kwa Kabuga na kurejeshwa Rwanda.

Hati hiyo ya mahakama inasema kwamba kutokana na matukio ya miaka miwili iliyopita, “Kabuga akiachiliwa atakwenda Rwanda pekee”.

Redio ya Ufaransa RFI inaripoti kwamba wakili wa Kabuga alijaribu kuuliza moja ya nchi za Ulaya kumkubali. Lakini , hata Ufaransa, nchi ambayo alikamatwa mwezi Mei, 2020 baada ya miaka 26 ya kuwa mafichoni haijakubali kumkaribisha.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment