Kuna mambo wamejaribu kufanya lakini hayaonekani kuzaa matunda,na kuna hali wanazipitia kiuchumi,kifamilia, kazini, na hawaamini tena Kama wanaweza kuvuka
Najua umezungukwa na watu wengi wanaokucheka na kukukatisha Tamaa kwasababu ya mambo unayoyapitia kwani hayaoneshi tumaini
Luka 18:27
Akasema, yasiyowezekana kwa wanadamu yawezekana kwa Mungu.
Mungu ameniinua ili kukutia moyo yasiyowezekana kwa wanadamu kwa Mungu yanawezekana usikate Tamaa,usife moyo songa mbele
Nimekuombea katika mwaka huu uliokubalika Mungu akafanye yale yoote yaliyoonekana hayawezekani kwenye maisha yako.
Na badala ya huzuni akakupe furaha, Badala ya machozi akakupe kicheko,badala ya kuzalauliwa akakuheshimishe.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.