Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Waziri Mkuu Donald Tusk amesema klichofanywa na Urusi kimevuka mstari mwekundu.

Poland inakaribia mzozo tangu Vita vya dunia vya pili – waziri Mkuu

Donald Tusk anasema Poland iko karibu zaidi kuanzisha mzozo kuliko wakati wowote tangu Vita vya Pili vya Dunia.
“Sina sababu ya kudai kwamba tuko ukingoni mwa vita, kwasababu mstari mwekundu umevukwa, na ni hatari zaidi kuliko hapo awali,” mawaziri wakuu wa Poland wameliambia bunge.
“Hali hii inatuleta karibu zaidi na mgogoro tangu Vita vya Pili vya Dunia”.
Wizara ya mambo ya ndani ya Poland imesema ndege saba zisizo na rubani za Urusi ziligunduliwa
Mamlaka nchini Poland imepata ndege saba zisizo na rubani na mabaki ya kitu kisichojulikana katika maeneo kote nchini kufuatia uvamizi wa anga ya Poland usiku kucha, msemaji wa wizara ya mambo ya ndani anasema.
Karolina Galecka anauambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba ndege tano zisizo na rubani na mabaki ya kitu kisichojulikana zilipatikana katika maeneo tofauti katika jimbo la Lublin, mashariki mwa Poland, ambayo inapakana na Belarus na Ukraine.
Anasema ndege zake mbili zisizo na rubani ziligunduliwa katikati na kaskazini mwa Poland, mbali zaidi na mipaka: Moja iligunduliwa katika shamba huko Mniszków, katika mkoa wa Łódź katikati mwa Poland, karibu kilomita 250 (maili 155) kutoka mpaka wa Belarusi.
Nyingine iligunduliwa karibu na jiji la Elbląg kaskazini mwa Poland
Qatar inasema ‘ina haki’ ya kujibu shambulizi la Israel

Qatar imezungumza na timu yake ya kisheria juu ya namna ya kumuwajibisha Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu kwa kuhusika na uvunjaji wa sheria za kimataifa.
Hapo jana, katika mkutano na waandishi wa habari, waziri mkuu wa Qatar alielezea shambulizi hilo kama “kitendo cha kigaidi cha serikali kilichofanywa chini ya Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu” na “ukiukaji wa uhuru”.
“Nchi ya Qatar ina haki ya kujibu mashambulizi ya Israel na itachukua hatua madhubuti dhidi ya ukiukaji wowote wa kizembe au uchokozi unaotishia usalama wake na utulivu wa kikanda,” taarifa ilisema.
Iliongeza kuwa wanaahidi kuchukua “hatua zote muhimu kujibu”.
Iliendelea kusema kuwa “Qatar itaanza mapitio ya kina ya sera na taratibu za kuzuia vitendo hivyo na kuzuia kujirudia.”
Urusi yasema haitatoa maoni yoyote kuhusu Poland
Kremlin imetoa maoni yake ya kwanza kuhusu Poland … ikisema haitatoa maoni.
“Hatungependa kutoa maoni juu ya hili,” alisema msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov kwenye mkutano wake wa kila siku na waandishi wa habari.
“Hili si la kwetu kufanya hivyo. Ni suala la wizara ya ulinzi [ya Urusi].”
Alipoulizwa kuhusu tuhuma zinazotolewa Moscow, Peskov anajibu: “Uongozi wa Umoja wa Ulaya na Nato unaituhumu Urusi kwa uchochezi kila siku, kwa kawaida bila kuunga mkono jambo hili.”
Ndege 24 za Urusi zisizo na rubani ziliingia Poland – Zelensky

Katika taarifa nyingine kutoka kwa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, kiongozi huyo anasema kuvuka kwa mpaka na kuingia Poland kwa ndege isiyo na rubani ya Urusi kulitokea saa 00:50 kwa saa za huko (23:50 BST).
Anaandika kwenye X kwamba “angalau ndege zisizo na rubani mbili za Urusi ambazo ziliingia katika eneo la Poland wakati wa usiku zilitumia anga ya Belarusi”.
Hii “inaweza kuwa kubwa kuliko takwimu iliyotangazwa hapo awali”, anasema. Kama ukumbusho, Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk amesema jeshi la Poland lilirekodi mashambulizi 19 ya ndege zisizo na rubani katika anga ya nchi hiyo usiku kucha.
Ndege zisizo na rubani “inavyoonekana” zilikuwa zikikaribia kushambulia Poland na vile vile Ukraine, anaongeza.
Anasema data iliyopatikana inaonyesha kuwa kulikuwa na angalau dazeni mbili za ndege zisizo na rubani za Urusi ambazo zingeweza kuingia kwenye anga ya Poland. Ukraine inafanya kazi katika kuthibitisha hili, anaongeza.
Majibu ya nchi za Magharibi hayatoshi kumfanya Putin kuogopa kutuma ndege zisizo na rubani nchini Poland

Huu ni mfano mwingine wa sera ya Magharibi ya iliofeli.
Kwa miaka mingi, majibu ya nchi za Magharibi kwa mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine yamekuwa yakidhibitiwa na hofu ya kuichokoza Moscow kufanya kitu kikali na cha ukatili zaidi.
Hofu hizi – pamoja na vikwazo vya kifedha – vimezuia washirika wa Ukraine kuipatia silaha nyingi na bora zaidi, achilia mbali kupeleka wanajeshi wa ardhini.
Lakini Kremlin haina wasiwasi kama huo. Imeweka uchumi wa Urusi kwenye msingi wa vita, na haiogopi kuongezeka kwa kuzidisha mashambulio ya anga dhidi ya Ukraine, kuwalenga raia, au kuwashirikisha wanajeshi wa Korea Kaskazini.
Majibu tuliyoyaona kutoka kwa nchi za Magharibi hadi sasa hayatoshi kumfanya Putin aogope matokeo iwapo ataamua kutuma ndege zisizo na rubani nchini Poland.
Maandamano ya Nepal ‘yaliingiliwa’ Gen Z wadai, huku jeshi likishika doria mitaani

Jeshi la Nepal limeshika doria katika mitaa ya mji mkuu Kathmandu, baada ya taifa hilo la kukabiliwa na machafuko mabaya zaidi kuwahi kutokea kwa miongo kadhaa.
Maandamano ya kupinga ufisadi na upendeleo serikalini yaligeuka na kuwa vurugu siku ya Jumanne.
Waziri mkuu alijiuzulu huku nyumba za wanasiasa zikiharibiwa, majengo ya serikali yakichomwa moto na bunge lilivamiwa na kuchomwa moto.
Lakini makundi ya vijana wa “Gen Z” yanayoongoza maandamano hayo yamejitenga na uharibifu huo, yakisema maandamano hayo “yalitekwa nyara na watu waliohisi wamepata “fursa” ya kufanya uharibifu.
Leo mitaa ya Kathmandu inaonekana kuwa tulivu, lakini moshi bado unafuka kutoka kwenye majengo yaliyochomwa moto huku magari yaliyoungua yakitapa barabarani.
Amri ya kutotoka nje imetangazwa kote nchini hadi Alhamisi asubuhi, jeshi lilisema, likionya kuwa hatua kali itachukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayejihusisha na ghasia hizo zilizosababisha uharibifu mkubwa.
Watu 27 wamekamatwa kwa kuhujihusisha na vurugu na uporaji. Silaha 31 pia zilichukuliwa kutoka mikononi mwa raia, iliongeza.
Jeshi linajaribu kudhibiti hali tete,baada ya Waziri Mkuu KP Sharma Oli kujiuzulu na kuacha ombwe la uongozi.
Mwanamke aliyemng’ata ulimi mshambuliaji wake aachiwa huru baada ya miaka 61

Mwanamke mmoja nchini Korea Kusini ameachiliwa huru baada ya mahakama kusikiliza upya kesi dhidi yake miongo kadhaa baada ya kuhukumiwa kifungo gerezani kwa kumng’ata ulimi mwanamume aliyemshambulia kingono.
Choi Mal-ja alikuwa na umri wa miaka 18 alipopatikana na hatia ya kumdhuru vibaya mshambuliaji wake na kuhukumiwa kifungo cha miezi 10 jela.
Mshambuliaji wake, ambaye alikuwa na umri wa miaka 21, alipokea kifungo chepesi cha miezi sita.
Kesi dhidi ya Choi ilianza kusikilizwa tena katika mji wa Busan mwezi Julai kufuatia kampeni ya muda mrefu iliyolenga kusafisha jina lake.
Katika kikao chao cha kwanza, waendesha mashtaka walimuomba msamaha na, katika hali isiyo ya kawaida, wakaiomba mahakama kufuta hukumu hiyo.
“Singeweza kuacha kesi hii iendelee bila kujibiwa… [nilitaka] kuwatetea waathiriwa wengine ambao wamejipata katika hali kama yangu,” Bi Choi alisema baada ya kuachiliwa.
Kesi ya Bi Choi imetajwa katika vitabu vya sheria nchini Korea Kusini kama mfano halisi wa mahakama kushindwa kubaini maana ya kujitetea wakati mtu anapokabiliwa na unyanyasaji wa kingono.
Kulingana na rekodi za mahakama, mshambuliaji huyo alikuwa amembamiza chini Bi Choi katika jaribio la kumbaka mahali huko Gimhae.
Alifanikiwa kujiokoa baada ya kung’ata na kukata takriban 1.5cm (0.59in) ya ulimi wake.
Mwanamume huyo alitaka kufidiwa jeraha alilopata katika kisa hicho na hata kuvunja nyumba ya Bi Choi wakati mmoja, vyombo vya habari vya Korea Kusini viliripoti.
Katika mojawapo ya maamuzi yenye utata zaidi nchini Korea Kusini kuhusu unyanyasaji wa kingono, mwanamume huyo alipewa kifungo cha miezi sita, baada ya kupatikana na hati aya kupitia njia ambayo hakustahili kupitia na kumtishia.
Hakuwahi kushtakiwa kwa jaribio la ubakaji. Bi Choi alipata adhabu kali zaidi kwa kumsababishia jeraha baya mwilini, huku mahakama ikisema wakati wa tukio hilo ikisema kuwa alivuka “mipaka ifaayo” ya kujilinda.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.