Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mwaka 1886 mfamasia John Pemberton ambaye kwa wakati huo alikuwa anajulikana kwa jina maarufu la Mr.Doc alikuwa amerudi kutoka vitani na akawa anawaza kujaribu tena baada ya kufeli mara kadhaa alitaka kugundua Kitu kitakachompa faida ya kibiashara.
.
Baada ya kufanya majaribio ndipo aligundua “formula” ya kikemikali ya kutengeneza kinywaji cha Coca-Cola na kwa kushirikiana na Frank Robinson walitengeneza logo na Kauli mbiu ya kwanza ya Coca-Cola ya “The Pause That Refreshes”.
.
Hata hivyo kwa mwaka mzima wa kwanza walifanikiwa kuuza chupa 25 tu ingawa kwa sasa wanauza zaidi ya chupa billioni 1.8 kwa siku.
.
Kanuni ya kuanza kidogo unaweza kuitumia kwenye Fedha,biashara na hata kazi unayofanya.Badala ya kudharau kidogo ulichonacho,jiulize:NITATUMIAJE KIDOGO NILICHONACHO KUPATA KIKUBWA NINACHOKITAFUTA?Je,wewe una Nini kidogo leo ambacho unaweza kuanza kukitumia?
.
Unavyoweza kupanga mpango wa kujipatia uhuru wa kifedha kwa kuanza na pesa,mtaji au kazi ndogo uliyonayo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.