Wanachama wa genge la waendesha baiskeli wanaopinga Uislamu wanaendesha ulinzi katika maeneo hatari ya misaada ya Gaza

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

g

Kampuni inayolinda maeneo ambayo misaada inasambazwa huko Gaza imekuwa ikiwatumia wanachama wa genge la waendesha baiskeli la Marekani wenye historia ya chuki dhidi ya Uislamu kuendesha usalama wao wenye silaha, uchunguzi wa BBC umegundua.

BBC News imethibitisha utambulisho wa wanachama 10 wa Klabu ya Pikipiki ya Infidels wanaofanya kazi huko Gaza la UG Solutions – mkandarasi binafsi anayetoa ulinzi katika maeneo ya Gaza Humanitarian Foundation, ambapo mamia ya raia waliokuwa wakitafuta chakula wameuawa katika matukio ya fujo na milio ya risasi.

Tunaweza kufichua kwamba wanachama saba wa genge hilo wako katika nyadhifa za juu za kusimamia maeneo kwenye operesheni yenye utata ya usaidizi inayoungwa mkono na Israel na Rais wa Marekani Donald Trump.

UG Solutions (UGS) ilitetea sifa za wafanyakazi wake kwa kazi hiyo, ikisema haichunguzi watu kwa “mapenzi ya kibinafsi au ushirika ambao hauhusiani na utendakazi wa kazi”.

Wakfu wa Misaada ya Kibinadamu wa Gaza (GHF) ulisema una “sera ya kutostahimili chuki yoyote, upendeleo wa kibaguzi au mienendo”.

Genge hilo kwa sasa linaandaa matamshi ya chuki dhidi ya Uislamu kwenye ukurasa wake wa Facebook na hapo awali limekuwa na nyama choma ya nguruwe “kukaidi” mwezi mtukufu wa Kiislamu wa Ramadhani.

Poland yadungua ndege zisizo na rubani za Urusi baada ya ‘ukiukaji mkubwa wa anga’

h

Taarifa ya jeshi la Poland imesema kuwa anga la nchi hiyo lilikiukwa mara kandhaa na ‘’vitu vinavyofanana na ndege zisizokuwa na rubani’’

Hii ilitokea wakati wa shambulio la hivi punde la Urusi kote Ukraine, ambapo shambulio la anga lilianza kabla ya usiku wa manane, na maonyo ya angalau droni 100 angani – na Urusi ikitayarisha makombora na kuyarusha.

Msemaji kutoka serikali ya Poland amesema mkutano wa dharura utafanyika saa nane alfajiri kwa saa za eneo na kuwa Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk tayari anakutana na mawaziri wanaohusika na usalama wa serikali kuhusu shambulio hilo.

Kisha, Waukraine walipoingia kwenye makazi chini ya ardhi, njia za mahandaki ambazo walitazama zilianza kuripoti ndege kadhaa zisizo na rubani zikivuka hadi Poland.

Walianza kuandika kwa lugha ya Kipoland, wakiwaonya watu huko kujificha. “Chelm – kwenye makazi!” , “Zamosc – ndani ya malazi!”

Hii inahisi kama kuongezeka kwa mashambulizi ya Moscow – kujaribu majibu ya Magharibi. Kwa sababu inaonekana ndege zake zisizo na rubani hazikuingia Poland tu.

Ziliingia ndani vya kutosha hata kusababisha uwanja wa ndege wa Warsaw kufungwa.

Na hii inatokea huku mashambulizi ya angani dhidi ya Ukraine yamekuwa makubwa zaidi na ya mara kwa mara.

Wikendi iliyopita, kombora la Urusi liligonga jengo kuu la serikali Poland. Kabla ya hapo, majengo ya EU na Baraza la Uingereza huko Kyiv yaliharibiwa.

Ndege zisizo na rubani za Urusi zimewahi kuvuka mpaka wa magharibi mwa Ukraine hapo awali. Kombora la Kirusi hata lilitua msituni mara moja, lakini halikulipuka.

Mnamo mwaka 2022, wanakijiji wawili waliuawa karibu na mpaka, inaonekana baada ya ulinzi wa anga wa Ukraine kuangusha kombora. Kwa hivyo jeshi la anga la Poland sasa lipo vitani.

Lakini hawajawahi kupiga kitu chochote hapo awali. Kwa hivyo hili ni eneo jipya kwa Poland na kwa Nato.

Qatar: Shambulio la Israeli ni ‘ugaidi wa serikali’ na tunayo haki ya kujibu

g
Maelezo ya picha,Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman bin Jassim Al Thani

Waziri mkuu na Waziri wa mambo ya jje wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman bin Jassim Al Thani ametangaza kwamba Qatar imekabiliwa na shambulio la “uhaini” la Israeli ambalo linaweza tu kuelezewa kama “ugaidi wa serikali.”

Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Doha, Al Thani alisisitiza kuwa nchi yake haitavumilia ukiukwaji wowote wa mamlaka yake na uadilifu wa eneo na itakabiliana kwa uthabiti na tisho lolote kwa usalama wake. Alithibitisha kuwa Qatar inayo haki ya kujibu “shambulio la wazi” na itachukua hatua zote muhimu kukabiliana nalo.

Waziri huyo alifichua kuwa Marekani iliifahamisha Qatar kuhusu shambulizi hilo dakika kumi baada ya kutokea, akibainisha kuwa Israel ilitumia silaha ambazo hazikugunduliwa na rada.

Alikitaja kile kilichotokea “jaribio la kuyumbisha usalama na utulivu wa kikanda,” akiongeza kuwa “Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu anaongoza eneo hilo kwa kiwango kisichoweza kurekebishwa,” na kwamba hatua hii imevuka viwango vyote vya maadili.

Al Thani alibainisha kuwa shambulio hilo limekuja licha ya mazungumzo yanayoendelea katika siku za hivi karibuni kwa ombi la Marekani kujadili mipango ya amani, ikiishutumu Israel kwa kujaribu kuhujumu juhudi hizo. Aliongeza, “Je, jumuiya ya kimataifa inahitaji ujumbe wa wazi zaidi kuhusu nani ni mnyanyasaji katika eneo hilo?”

Waziri huyo alisisitiza kuwa Qatar haijaacha juhudi zozote za kusimamisha vita huko Gaza, lakini baada ya shambulio la hivi karibuni, haoni uwezekano mkubwa wa kupatikana kwa makubaliano ya amani.

Aliongeza, “Diplomasia ya Qatar imejengwa juu ya misingi ya utulivu na suluhu za kisiasa, na hakuna kitendo cha uadui kitakachotuzuia kuendelea na jukumu letu la upatanishi na kujitahidi kuleta utulivu wa kikanda.”

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment