Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kuna mambo nimejifunza kwenye maisha unapopitia hali ngumu…
Nilichogundua ni kuwa unapopitia hali hiyo unasikia maumivu lakini baada ya kutoka unashukuru kuwa ulipitia.
Wakati huu unaitwa, wakati wa kutengenezwa (Season of Construction).
Kuna mambo unapitia sio kwa sababu Mungu amekuacha ama hakuna njia ya kutoka.
Ila unapitia ili kukusaidia kuwa bora zaidi kwa hatua inayofuata.
1. Kuna wakati unakuwa unafanya kila Kitu lakini hakuna Kitu kinachosogea.
Wakati huu inapimwa “Passion” yako.
Mafanikio yameandaliwa kwa watu ambao wanamaanisha na hawako tayari kukatishwa tamaa.
NI wakati wako wa KUTENGENEZWA.
2. Kuna wakati watu ambao umewatendea mema wanakugeuka ama hawapatikani wakati unawahitaji.
Hapa unapimwa moyo wako wa KUSAMEHE wanaokukosea.
Huwezi kufika mbali kama kila anayekukosea ama kukuacha anageuka kuwa adui.
Ni wakati wako wa KUTENGENEZWA.
3. Kuna wakati UTASHAMBULIWA na KUFANYIWA hila na watu wanaotamani anguko lako.
Mungu atahakikisha UNAWAFAHAMU kwa wazi kabisa.
Na wengine watafanya waziwazi.
Hapa unapimwa uwezo wako wa “KUFOCUS”
– Huwezi kufika mbali kama kila anayekutupiwa jiwe unataka kuliokota mrushie.
Ni wakati wako wa KUTENGENEZWA.
4. Kuna wakati unaamua kufuatilia Kitu na Unaamini kabisa kuwa ni cha KWAKO kwa 100% lakini kwa namna usiyoielewa unashindwa kukipata.
Na kila mtu aliyekuwa anasimama na wewe anakuacha peke yako.
Hapa unapimwa uwezo wako wa kujiamini kuwa UNAWEZA KUINUKA TENA BAADA YA KUANGUKA.
Kwenye MAISHA uwezo wako wa KUINUKA tena baada y KUANGUKA ni wa MUHIMU SANA ili ufanikiwe tena.
Ni wakati wako wa KUTENGENEZWA.
Je, umeshapitia wakati huu ama unaupitia sasa?
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.