Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Hamas yadai viongozi wa Hamas wamenusurika na shambulio lake mjini Doha, huku Trump akisema hajafurahi

Hamas imedai imesema kuwa viongozi wake waliolengwa na shambulizi la anga la Israel wamenusurika , lakini watu sita wameuawa katika shambulio hilo.
Wakati huo huo Rais wa Marekani Donald Trump amesema “hajafurahishwa” na mashambulizi ya anga ya Israel huko Qatar, na kuongeza shinikizo la kimataifa baada ya kuongezeka kwa vita vya Israel dhidi ya Hamas.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema mashambulizi hayo yalikuwa “halali kabisa” kwa sababu uyaliwalenga viongozi wakuu wa Hamas ambao walipanga shambulio la tarehe 7 Oktoba 2023 dhidi ya Israeli, ambalo lilianzisha vita vya Gaza.
Kundi la wapiganaji wa Palestina limesema wanachama wake watano waliuawa katika shambulio la anga la Israel katika mji mkuu wa Qatar, lakini lilidai kuwa jaribio la kuua timu yake ya mazungumzo “lilifeli”.
Qatar ililaani shambulizi hilo la Israel, na kuliita la “uoga” na “ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa”.
Qatar ni mshirika mkuu wa Marekani katika eneo ambalo ni eneo la kituo kikuu cha anga cha Marekani.
Alipoulizwa kuhusu mashambulizi ya Israel dhidi ya Qatar, Trump alisema: “Sawa, sifurahishwi… sijafurahishwa na hali nzima. Sio hali nzuri.
“Lakini nitasema hivi, tunataka mateka warejeshwe, lakini hatujafurahishwa na jinsi ilivyoshuka leo,” aliambia vyombo vya habari.
Hamas ilisema timu ya mazungumzo ilikuwa inakutana kujadili pendekezo la hivi punde la Marekani la kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza katika makazi ya watu huko Doha wakati liliharibiwa vibaya na mfululizo wa milipuko.
Wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo ya Ghuba imesema mwanajeshi mmoja wa kikosi chake cha Usalama wa Ndani aliuawa na wengine kujeruhiwa, bila kutaja majeruhi wowote wa Hamas.
Qatar imekuwa mwenyeji wa ofisi ya kisiasa ya Hamas tangu 2012, na imehudumu pamoja na Marekani na Misri kama mpatanishi katika mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya kundi hilo na Israel
Hamas imesema kuwa viongozi wake waliolengwa na shambulizi lake la anga katika mji mkuuu wa Qatar Doha wamenusurika , lakini watu sita wameuawa katika shambulio hilo.
Qatar: Shambulio la Israeli ni ‘ugaidi wa serikali’ na tunayo haki ya kujibu

Waziri mkuu na Waziri wa mambo ya jje wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman bin Jassim Al Thani ametangaza kwamba Qatar imekabiliwa na shambulio la “uhaini” la Israeli ambalo linaweza tu kuelezewa kama “ugaidi wa serikali.”
Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Doha, Al Thani alisisitiza kuwa nchi yake haitavumilia ukiukwaji wowote wa mamlaka yake na uadilifu wa eneo na itakabiliana kwa uthabiti na tisho lolote kwa usalama wake. Alithibitisha kuwa Qatar inayo haki ya kujibu “shambulio la wazi” na itachukua hatua zote muhimu kukabiliana nalo.
Waziri huyo alifichua kuwa Marekani iliifahamisha Qatar kuhusu shambulizi hilo dakika kumi baada ya kutokea, akibainisha kuwa Israel ilitumia silaha ambazo hazikugunduliwa na rada. Alikiitaja kile kilichotokea “jaribio la kuyumbisha usalama na utulivu wa kikanda,” akiongeza kuwa “Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu anaongoza eneo hilo kwa kiwango kisichoweza kurekebishwa,” na kwamba hatua hii imevuka viwango vyote vya maadili.
Al Thani alibainisha kuwa shambulio hilo limekuja licha ya mazungumzo yanayoendelea katika siku za hivi karibuni kwa ombi la Marekani kujadili mipango ya amani, ikiishutumu Israel kwa kujaribu kuhujumu juhudi hizo. Aliongeza, “Je, jumuiya ya kimataifa inahitaji ujumbe wa wazi zaidi kuhusu nani ni mnyanyasaji katika eneo hilo?”
Waziri huyo alisisitiza kuwa Qatar haijaacha juhudi zozote za kusimamisha vita huko Gaza, lakini baada ya shambulio la hivi karibuni, haoni uwezekano mkubwa wa kupatikana kwa makubaliano ya amani. Aliongeza, “Diplomasia ya Qatar imejengwa juu ya misingi ya utulivu na suluhu za kisiasa, na hakuna kitendo cha uadui kitakachotuzuia kuendelea na jukumu letu la upatanishi na kujitahidi kuleta utulivu wa kikanda.”
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.