Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Zelensky alaani ‘shambulio la kikatili’ baada ya Urusi kulishambulia jengo kuu la serikali katika jimbo la Kyiv

Jengo kuu la serikali ya Ukraine huko Kyiv limepigwa kwa mara ya kwanza katika vita wakati wa mashambulizi ya Urusi, waziri mkuu wa Ukraine amesema.
Yulia Svyrydenko alisema paa la jengo hilo na gorofa la juu vimeharibiwa kwa moto “kwasababu ya shambulio la adui”.
Takriban watu wanne waliuawa katika shambulio hilo kote nchini, akiwemo mtoto mchanga na mwanamke kijana waliofariki baada ya jengo la makazi la ghorofa tisa kugongwa katika wilaya ya Svyatoshynsky ya Kyiv, maafisa walisema.
Jeshi la anga la Ukraine liliripoti kuwa idadi kubwa ya ndege zisizo na rubani na makombora zilizinduliwa na Urusi katika shambulio la hivi punde la usiku – zaidi ya 800 kwa jumla.
Kulingana na jeshi la anga, makombora tisa na ndege zisizo na rubani 56 vilishambulia maeneo 37, na vifusi vya ndege zisizo na rubani viliangukia katika maeneo manane.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema msururu huo wa mashambuliz ulisababisha uharibifu katika miji ya Zaporizhzhia, Kryvyi Rih na Odesa, na pia katika mikoa ya Sumy na Chernihiv.
“Mauaji kama haya sasa, wakati ambapo diplomasia ya kweli ingeweza kuanza muda mrefu uliopita, ni uhalifu wa makusudi na jaribio la kurefusha vita,” Zelensky alisema kwenye mitandao ya kijamii, akihimiza utashi wa kisiasa kutoka kwa ulimwengu kukomesha mashambulizi hayo.
Wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema imefanya mashambulizi kwenye jengo la kijeshi na viwanda la Ukraine na miundombinu ya usafirishaji, na kusababisha uharibifu kwenye maghala ya silaha na vifaa vya kijeshi.
Zelensky: Putin alipata kile alichotaka katika mkutano wa Alaska na Trump

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameliamba shirika la habari la ABC kwamba mkutano wa Rais Donald Trump na Rais wa Urusi Vladimir Putin uliofanyika Alaska ulimpa kiongozi wa Urusi Vladimir Putin kile alichotaka.
“Ni aibu kwamba Ukraine haikuwepo kwasababu nadhani Rais Trump alimpa Putin kile alichotaka,” Zelensky alisema. “Alitaka sana kukutana na Rais Trump, na rais wa Marekani. Na nadhani Putin alifikia hilo . Na hiyo ni aibu.”
Zelensky alifanya mahojiano na mwandishi mkuu wa masuala ya kimataifa wa ABC News Martha Raddatz siku ya Ijumaa, ambayo yalitangazwa i kwenye kipindi cha ABC News “Wiki hii.”
“Putin hataki kukutana nami, lakini anataka kukutana na rais wa Marekani ili kuonyesha kila mtu video na picha za uwepo wake,” rais wa Ukraine alisema.
Akizungumzia uwezekano wa kukutana na Putin, Zelensky alisema kuwa rais wa Urusi alikuwa ametoa masharti ya mkutano huo ambayo hangeweza kuyakubali na kwamba Putin “alikuwa akicheza michezo na Marekani.”
“Alisema alisema atakutana nawe kama utakuja Moscow,” Raddatz alimwambia Zelensky.
Zelensky alicheka. “Anaweza kuja Kyiv,” alisema, na kuongeza: “Siwezi kwenda Moscow wakati nchi yangu inapigwa na roketi na mashambulizi kila siku.”
Raddatz alipouliza ni nini angechukulia kuwa ushindi kwa nchi yake, Zelensky alijibu kwamba ni kuishi kwa Ukraine.
“Lengo la Putin ni kuikalia Ukraine,” Zelensky alisema. “[Putin] hakika anataka kutuchukua kabisa. Kwake, huo ni ushindi. Na hadi afanye hivyo, ushindi uko upande wetu. Kwa hivyo kwetu, kuishi ni ushindi. Kwasababu tunaishi kwa kuhifadhi utambulisho wetu, nchi yetu, uhuru wetu.”
Kupatwa kwa Mwezi 2025: Tazama Mwezi wa Mwekundu ulivyoonekana ulimwenguni kote

Watazamaji kote ulimwenguni wamekuwa wakishuhudia Mwezi wa Damu (Blood Moon) unaovutia – jambo ambalo hutokea wakati Mwezi unapita kwenye kivuli cha dunia, na kuwa na rangi nyekundu.

Katika nchi kadhaa ulimwenguni mwezi huo ulionekana kwa ukamilifu huku baadhi ya maeneo yakiona sehemu ya mwezi huo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.