Uwezo wa Mungu ni mkuu.

Daudi hakuhitaji kujua uwezo wa Goliath ili kumkabili ila alitiwa nguvu baada ya kujua uwezo wa Mungu aliyenaye

Kwanini kila siku unashindwa?
Kwanini kila siku wewe ni mtu wa kulia?

Nikwasababu unaangalia ukubwa wa vita uliyonayo,ukubwa wa jaribu ulilonalo,ukubwa wa tatizo ulilonalo badala ya kuangalia uwezo wa Mungu uliyenaye.

Mwamini Mungu uliyenaye, amini uwezo wake, amini juu ya ahadi zake, usiamini tatizo ulilonalo au changamoto ulizo nazo hizo ni za muda tu

Ndio maana Daudi alimwambia Goliath mimi nakujia kwa jina la Bwana wa majeshi

1samweli 17:45 Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la BWANA wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana.

Daudi hakuangalia ukubwa wa Goliath,alitazama ukubwa wa Mungu aliyenaye

Kwanini wewe unaangalia ukubwa wa tatizo ulilonalo? Kwanini ukubwa wa changamoto yako ukufanye umuone Mungu wako dhaifu?

Mwamini Mungu na ninakuombea Mungu unamtegemea akakuikoe wakati wa mateso na uitapo akakuitikie


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment