Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Huwezi kuwa na mtazamo CHANYA kwenye maisha kama wewe kila siku una jicho la kuona MABAYA tu.
Umeshawahi kuwa na mtu kwenye mahusiano halafu kila siku anakukosoa kwa mabaya lakini hata hukumbuki mara ya mwisho akisifia ZURI ulilolifanya?
.
Au kuna mtu uko naye ofisini kila siku ni kusema kwa sauti mambo yanapoenda mrama ila hajawahi hata “kuapreciate” kitu kizuri?
.
Njia mojawapo ya kujenga mtazamo chanya (Positive Attitude) kwenye maisha yako ni kujilazimisha kutafuta vitu vya KUSIFIA na KUSHUKURU.
Hata katikati ya MAGUMU unatakiwa kutafuta jambo ambalo linaweza kukusababisha kushukuru na kusifia.
Ukweli ni kuwa kila siku kuna kitu ambacho unaweza kukipata na ukashukuru au ukasifia.
Ila UTAKIONA tu kama UTAKITAFUTA.
Leo anza kutafuta kitu cha kushukuru kwanza.
Kisha tafuta angalau watu WATATU ambao utawaambia maneno mazuri ya KUWASIFIA na KUWATIA MOYO.
Mara nyingi tunadhani tukifanya hivyo TUNAWASAIDIA wao ila ukweli ni kuwa TUNAJIJENGA wenyewe MTAZAMO CHANYA.
Leo unaanza kushukuru kwa jambo gani?
Ukipata mtu wa kumsifia au kumwambia maneno mazuri, Usisahau kunipa MREJESHO.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.