Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Bila kujali jana imekuwa mbaya kiasi gani na imekukosesha furaha au hata umekosa usingizi, leo ni siku mpya, anza kwa kuamini katika KUWEZEKANA.
2. Sitapoteza Furaha Yangu:
Ukipoteza furaha unapoteza nguvu ya kusonga mbele.
Usiruhusu maneno ya watu, hali ngumu unayoipitia ama kuumizwa moyo kukunyang’anye furaha.
Unachopitia ni cha Muda mfupi, ANGALIA KUZURI unakokwenda na SAHAU MABAYA YALIYOPITA.
3. Sitalaumu, Sitalalamika: Mambo haya mawili ni sababu kubwa ya kuufanya ubongo wako usifanye kazi kwa ufanisi.
Unapolaumu ama kulalamika unauambia ubongo wako kuwa UMESHINDWA kupata suluhisho na hivyo unaua nguvu yako ya ubunifu.
Jaribu kutolaumu au kutolalamika kwa siku nzima leo na utaona tofauti yake.
Umeshajiambia Mambo Haya Matatu?
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.