Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Onyo hilo limewadia baada ya waziri mwenye msimamo mkali wa Israel kufichua pendekezo la kutwaliwa kwa takriban theluthi nne za Ukingo wa Magharibi.
Umoja wa Falme za Kiarabu umeionya Israel kwamba kutwaa Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu ” kutavuka mpaka” na kudhoofisha ari ya Mkataba wa Abraham ambao ulirejesha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Afisa mkuu wa Imarati, Lana Nusseibeh, alisema hatua hiyo itakuwa mwisho wa kutafuta suluhisho kwa mataifa hayo mawili katika mzozo wa Israel na Palestina.
Wizara ya mambo ya nje ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina imesema inakaribisha msimamo wa UAE.
Serikali ya Israel haijatoa maoni yoyote. Lakini matamshi ya Nusseibeh yalikuja baada ya Waziri wa Fedha mwenye msimamo mkali Bezalel Smotrich kufichua pendekezo la kutwaliwa kwa takriban theluthi nne za Ukingo wa Magharibi.
Israel imejenga takriban makazi 160 ya Wayahudi 700,000 tangu ilipoikalia kwa mabavu Ukingo wa Magharibi na Jerusalem Mashariki – ardhi ambayo Wapalestina wanataka, pamoja na Gaza, kwa taifa linalotarajiwa – wakati wa vita vya Mashariki ya Kati vya 1967. Takriban Wapalestina milioni 3.3 wanaishi kando ya eneo hilo..
Makazi hayo ni kinyume cha sheria chini ya sheria za kimataifa.
Israel yazidisha mashambulizi katika mji wa Gaza

Vikosi vya Israel vinazidisha mashambulizi yao kwenye viunga vya Mji wa Gaza, wakaazi wanasema, huku wanajeshi wakiongeza maandalizi ya mashambulizi ya ardhini ili kuuteka mji huo.
Hospitali zilisema wanawake na watoto ni miongoni mwa zaidi ya Wapalestina 30 waliouawa katika mashambulizi ya Israel katika mji huo siku ya Jumatano, wengi wao kaskazini na magharibi.
Mkuu wa majeshi wa Israel aliapa “kuendelea kushambulia vituo vya Hamas kwa nguvu yote hadi itakaposhindwa” na mateka wake kuachiliwa.
Umoja wa Mataifa na mashirika ya kutoa misaada yalisema operesheni za Israel tayari zilikuwa na “athari mbaya za kibinadamu” kwa familia zilizokimbia makazi yao katika mji huo, ambao ni makazi ya watu milioni na ambapo njaa ilitangazwa mwezi uliopita.
Wakati huo huo, waandamanaji wa Israel walishiriki katika kile walichokiita “siku ya kuvuruga” kuishinikiza serikali yao kukubaliana mara moja makubaliano ambayo yatamaliza vita ili kuachiliwa huru mateka wote 48 wa Israel na wa kigeni huko Gaza, 20 kati yao wanaaminika kuwa hai.
Uingereza na washirika wake wako tayari kuunga mkono Ukraine

Uingereza na washirika wake wako tayari kuunga mkono Ukraine kabla ya mazungumzo ya kumaliza vita na hatimaye kufikia makubaliano ya amani, waziri wa ulinzi wa Uingereza anasema.
Katika mkesha wa mkutano wa ngazi ya juu mjini Paris, John Healey aliiambia BBC mjini Kyiv kwamba washirika wa Ukraine “watasaidia kufanya anga, bahari kuwa salama, na kulinda ardhi”, mara tu makubaliano ya amani yatakapofikiwa.
Lakini muda mfupi kabla ya hapo, Rais wa Urusi Vladimir Putin alikuwa amewasilisha ujumbe wa dharura kutoka China, akiapa kwamba uvamizi wake kamili unaweza kuendelea.
Healey alipendekeza kwamba kulikuwa na vitisho katika maneno ya Putin, akisisitiza kuwa Urusi ilikuwa chini ya shinikizo.
Pia alimsifu Rais wa Marekani Donald Trump ambaye alisema “alimleta Putin kwenye mazungumzo” na bado “hajashikilia msimamo wowote”, licha ya ukosoaji mkubwa wa makaribisho mazuri ambayo Trump alimpa kiongozi huyo wa Urusi mwezi uliopita huko Alaska.
Alipoulizwa Jumatano ikiwa vita vya Ukraine vinaweza kumalizika hivi karibuni, Putin alisema “kuna matumaini ya kufaulu”.
“Kwangu ninaona busara ikitawala, kuna uwezekano wa kukubaliana juu ya suluhu la kumaliza mzozo huu,” alisema, kabla ya kutishia: “Ikiwa sivyo, basi itabidi kutatua tuliyonayo kijeshi.”
Waathiriwa wa Epstein kuandaa orodha ya walioathirika na unyanyasaji wa kingono

Waathiriwa wa Jeffrey Epstein wameshirikisha madhila waliopitia ya unyanyasaji wa kingono walipokuwa wakizungumza katika eneo la Bunge la Marekani na kutoa wito kwa wabunge kutoa faili zaidi kuhusu kashfa ya ngono ya Epstein ambaye alipatikana na hatia.
Mmoja wa wanawake hao, Lisa Phillips, alisema kundi hilo limeanza kuandaa orodha ya siri ya waathiriwa wa Epstein ambao wanasema walinyanyaswa.
“Tutakusanya kwa siri majina ambayo sote tunajua yalikuwa mara kwa mara katika ulimwengu wa Epstein,” alisema. Kazi hiyo “itafanywa na walionusurika kwa ajili ya walionusurika.”
Hafla hiyo iliandaliwa na wabunge wa Marekani ambao wanataka faili zaidi za uchunguzi wa Epstein zitolewe hadharani.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.