Xi apongeza ‘China isioweza kuzuilika’ na kuzindua silaha mpya kuonyesha nguvu yake

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

XI aonyesha nguvu ya kijeshi ya China na kidiplomasia katika hafla ya gwaride la heshima ambayo inaashiria miaka 80 ya kujisalimisha kwa Japan katika Vita vya Pili

kuonyesha nguvu yake

.

Rais wa China Xi Jinping ameonya kwamba ulimwengu unakabiliwa na chaguo kati ya amani au vita wakati akifanya gwaride kubwa zaidi la kijeshi nchini mwake Jumatano, akiwa na Vladimir Putin wa Urusi na Kim Jong Un wa Korea Kaskazini.

“Leo, binadamu anakabiliwa na chaguo la amani au vita, mazungumzo au mzozo, ushindi kwa pande zote mbili au upande mmoja,” Xi aliambia umati wa watazamaji zaidi ya 50,000 huko Tiananmen Square, na kuongeza kuwa watu wa China “wanasimama upande stahiki wa historia”.

Wakati wa gwaride hilo China imeonyesha silaha ikiwa ni pamoja na ya laser ya LY-1 ambayo iliwekwa juu ya lori la kivita la Wheeler Hz-155.

Silaha hii ya laser inasemekana kuwa na nguvu sana na inaweza kulemaza au kuchoma vifaa vya kielektroniki, au hata kuziba marubani, alisema mchambuzi wa utetezi Alexander Neill.

Tukio hilo la kifahari la kuadhimisha miaka 80 tangu kushindwa kwa Japan mwishoni mwa Vita vya Pili vya Dunia limeepukwa kwa kiasi kikubwa na viongozi wa Magharibi, kutokana na vita vya Ukraine na msimamo wa Kim juu ya silaha za nyuklia.

Ni mara ya kwanza viongozi watatu wote kuonekana pamoja hadharani huku wengine zaidi wakijiunga nao.

Video: Tazama China ikionesha uwezo wake wa kijeshi katika gwaride

Maelezo ya video,Uwezo wa kijeshi wa China

Rais Xi Jinping alionesha uwezo wa kijeshi wa China na kuzindua silaha mpya wakati wa gwaride mjini Beijing, kuadhimisha miaka 80 tangu Japan kujisalimisha katika Vita vya Pili vya Dunia.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi wa dunia akiwemo rais wa Urusi Vladimir Putin kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.

Maelfu ya wanajeshi wa akiba wa Israel wafika kazini kabla ya kushambulia mji wa Gaza

.

Maelfu ya wanajeshi wa akiba wameanza kuripoti kazini huku jeshi la Israel likiendelea na mikakati yake kufanya mashambulizi ya kuuteka mji wa Gaza.

Vikosi vya ardhini tayari vinasonga mbele katika viunga vya eneo kubwa zaidi la mjini Gaza, ambalo jeshi limesema ni ngome ya Hamas.

Mji huo pia unakabiliwa na mashambulizi makubwa ya anga na mizinga ya Israel, huku hospitali za eneo hilo zikisema kuwa zaidi ya Wapalestina 50 wameuawa tangu usiku wa manane.

Jeshi limewaamuru wakaazi kuhama na kuelekea kusini mara moja. Umoja wa Mataifa unasema takriban 20,000 wamefanya hivyo katika muda wa wiki mbili zilizopita, lakini karibu milioni wamesalia.

Marekani yashambulia meli iliyobeba dawa za kulevya

.

Rais Donald Trump anasema Marekani imeshambulia meli ya kubeba dawa za kulevya kusini mwa Karibea, na kuwauwa “mabwanyenye 11 wa ulanguzi wa dawa za kulevya “.

Alichapisha kwenye mitandao ya kijamii kwamba operesheni ya kijeshi ya Marekani Jumanne iliwalenga wanachama wa genge la Venezuela la Tren de Aragua.

.

Trump alisema meli hiyo ilikuwa katika maji ya kimataifa ikisafirisha mihadarati iliyokuwa ikielekea Marekani.

Utawala wa Trump umeongeza shinikizo za kijeshi na kisiasa dhidi ya Rais wa Venezuela Nicolas Maduro katika wiki za hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na kutoa zawadi ya $50m (£37m) kwa atakayetoa taarifa zitakazopelekea kukamatwa kwake kwa tuhuma za ulanguzi wa dawa za kulevya.

Maduro ameapa Venezuela itapambana na jaribio lolote la kuingilia kijeshi la Marekani.

Ahukumiwa kifo kwa kumchoma moto mkewe akiwa hai kwa rangi yake

.

Onyo: Makala haya yana maelezo ambayo yanaweza kuwa ya kuhuzunisha.

Mahakama nchini India imetoa hukumu ya kifo kwa mwanamume mmoja kwa kumchoma moto mkewe akiwa hai kwa sababu ya ubaguzi wa rangi.

Katika taarifa zake kabla ya kifo chake, Lakshmi alisema kwamba mumewe Kishandas “mara kwa mara alimdhihaki kwa kuwa na ngozi nyeusi”.

Jaji wa Wilaya Rahul Choudhary katika mji wa kaskazini wa Udaipur alielezea hukumu ya kifo akisema mauaji yaliyotekelezwa ni “nadra sana” na “ni uhalifu dhidi ya binadamu”.

Wakili wa Kishandas aliambia BBC kuwa mteja wake hana hatia na kwamba watakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Mauaji ya Lakshmi miaka minane nyuma na hukumu iliyotolewa mwishoni mwa juma, yamegonga vichwa vya habari katika nchi ambayo inashuhudia visa vingi vya ubaguzi wa rangi.

Shambulizi hilo dhidi ya Lakshmi lilifanyika usiku wa tarehe 24 Juni 2017, kulingana na amri ya mahakama iliyoonekana na BBC.

Hukumu hiyo inanukuu taarifa ambazo mwanamke huyo alizitoa kabla ya kifo chake kwa polisi, madaktari na hakimu mtendaji.

Lakshmi alisema mumewe mara nyingi alimwita “kali” au ngozi nyeusi na kumwaibisha tangu walipofunga ndoa yao mnamo 2016.

Xi apongeza ‘China isioweza kuzuilika’ na kuzindua silaha mpya

Mahakama yamuondolea Cardi B mashtaka ya kumshambulia mlinzi huko Los Angeles

.

Mwanamuziki nyota wa muziki wa Pop, Cardi B amepata ushindi mahakamani dhidi ya mlinzi aliyewasilisha kesi ya dola milioni 24 akimtuhumu mwimbaji huyo ambaye alikuwa mjamzito wakati huo kwa kumpiga kimwili nje ya ofisi ya daktari wa masuala ya uzazi huko Beverly Hills mwaka 2018.

Majaji 12 wa Mahakama ya Juu ya Los Angeles walijadili kwa chini ya saa moja kabla ya kufikia uamuzi wa pamoja uliomuunga mkono msanii huyo mwenye umri wa miaka 32, aliyeshinda tuzo ya Grammy, ambaye nyimbo zake zilizovuma ni pamoja na “Taki Taki” na “I Like It.”

Majaji waligundua kuwa mlinzi huyo wa zamani Emani Ellis, alishindwa kuthibitisha kwa uthabiti madai kwamba Cardi B alimshambulia kimwili na kumkwaruzwa usoni kwa kucha, akamtemea mate na kumrushia maneno makali ya ubaguzi wa rangi. Wanawake wote wawili ni Weusi.

Ellis alitoa ushahidi wakati wa kesi hiyo kwamba alimtaka Cardi B kuondoka kwenye maeneo ya jengo hilo la matibabu kwa sababu “alisababisha usumbufu.”

Akitoa shahidi katika utetezi wake mwenyewe, Cardi B alieleza kuwa Ellis ndiye mchokozi katika kile mwimbaji huyo alichoita “mabishano ya maneno” ambayo yalianza wakati Ellis, ambaye wakati huo alikuwa kazini akiwa amevaa sare yake, alipoanza “kuingilia faragha yangu.”

Kulingana na Cardi B, Ellis alianza kumfuata na kujaribu kumchukua video mwimbaji huyo alipokuwa akienda kwa daktari wa masuala ya uzazi alipokuwa mjamzito lakini alikuwa bado mwenyew

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment