Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Klabu ya Arsenal imekamilisha usajili wa beki Piero Hincapié (23) raia wa Ecuador kwa mkataba wa mkopo wenye jukumu la kumnunua jumla Juni 2026 kwa Euro milioni 52 akitokea Bayer Leverkusen.

Klabu ya Manchester United Fc imethibitisha kumsajili mlinda mlango Senne Lammens kwa ada ya uhamisho ya Euro milioni 21 pamoja na nyongeza akitokea Royal Royal Antwerp Fc ya Ubelgiji.
Lammens (23) raia wa Ubelgiji amesaini mkataba wa miaka mitano utakaombakisha klabuni hapo mpaka Juni 2030.
Klabu ya Newcastle United imethibitisha kumsajili mshambuliaji Yoane Wissa kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 55 akitokea Brentford, dili ambalo limekamilika dakika 30 kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili la majira ya kiangazi.
Wissa (28) mzaliwa wa Ufaransa ambaye anachezea timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amesaini mkataba wa miaka minne utakaombakisha klabuni hapo mpaka Juni 2029.
Nyota huyo wa zamani wa FC Lorient ya Ufaransa anatua Newcastle United huku akikabiliwa na jukumu la kuvaa viatu vya Alexander Isak aliyetimkia Liverpool.
Klabu ya Tottenham Hotspur imekamilisha usajili wa mshambuliaji Randal Kolo Muani (26) kwa mkataba wa mkopo sio na chaguo la kumnunua jumla akitokea Paris Saint-German.
Spurs itailipa PSG ada ya mkopo ya Euro milioni 5 huku ikiwajibika kulipa mshahara wote wa nyota huyo raia wa Ufaransa kwa kipindi chote cha mkopo huo.

Aston Villa hawakupokea ofa kutoka Manchester United kwa ajili ya kipa wa Argentina Emiliano Martinez licha ya mchezaji huyo mwenye miaka 32 kuhusishwa sana na uhamisho wa kuelekea Old Trafford. (Sky Sports)
Manchester United waliamua kutomchukua Martinez kwa sababu ya umri wake na mshahara unaokaribia pauni 200,000 kwa wiki. (Mirror)
Martinez hakuwa na hamu ya kujiunga na Galatasaray licha ya ripoti kutoka Uturuki kuhusu ofa ya thamani ya pauni milioni 21.6. (Daily Mail)
Liverpool walikataa kumruhusu Joe Gomez, 28, kujiunga na AC Milan baada ya mpango wao wa kumsajili beki wa England Marc Guehi, 25, kutoka Crystal Palace kuvunjika. (Fabrizio Romano)
Video ya kuaga ya Guehi kutoka Crystal Palace ilivuja mitandaoni lakini bado ameridhika kumalizia mwaka mmoja wa mkataba wake Selhurst Park na kisha kuondoka bure msimu ujao wa kiangazi. (Talksport)

Marc Guehi
Bayern Munich walitaka kumsajili mshambuliaji wa Nigeria Ademola Lookman, 27, kutoka Atalanta kwa mkopo siku ya mwisho ya dirisha la usajili. (Sky Sports)
Mshambuliaji wa Kiingereza wa Chelsea Raheem Sterling anaonekana kubaki Stamford Bridge kwani hakuna timu kutoka Uturuki, Saudi Arabia au Marekani zilizoonyesha nia ya kumsajili nyota huyo mwenye miaka 30 hata kama madirisha yao ya usajili bado yako wazi. (The Athletic)
Crystal Palace walijiondoa katika mpango wa mkopo wa mshambuliaji wa Tottenham, Manor Solomon, 26, kutoka Israeli licha ya kuwepo kibali kilichowaongezea muda wa kukamilisha usajili huo. (Sky Sports)

Uhamisho wa kiungo wa Wales Harry Wilson kutoka Fulham kwenda Leeds ulivunjika baada ya Fulham kubadili uamuzi dakika za mwisho kuhusu kumuuza mchezaji huyo mwenye miaka 28. (Yorkshire Evening Post)
Kuvunjika kwa uhamisho wa Wilson pia kulihitimisha uwezekano wa Chelsea kumpeleka Fulham kwa mkopo winga wa Kiingereza Tyrique George mwenye miaka 19. (Evening Standard)
Mshambuliaji wa Denmark Will Osula, 22, atabaki Newcastle United licha ya kuvutiwa na Eintracht Frankfurt waliotaka kumsajili kwa mkopo wa msimu mzima siku ya mwisho ya dirisha la usajili. (Athletic)
Vyanzo vya ndani vya Newcastle United vimesema mshambuliaji wa Sweden Alexander Isak, 25, alikuwa akicheza na kuonyesha tabia kana kwamba hataki timu hiyo ifuzu Ligi ya Mabingwa kuanzia mwezi Aprili. (Telegraph)
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.