Wachongaji Augustino na Antonio ni waliopata kazi kuchora sanamu ya mfalme Daudi

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Augustino na Antonio ni wachongaji maarufu wa kiitaliano ambao walitangulia kupewa kazi ya kuchonga sanamu ya…

…mfalme Daudi kutoka kwenye jiwe lililokuwa limechaguliwa (Marble) kati ya miaka 1464-1475.

Hata hivyo hawakuweza kukamilisha kwa sababu walisema jiwe lile halifai kwa kuchonga sanamu nzuri.

Baada ya miaka 25 kazi hiyo ilikabidhiwa kwa Michangelo na alianza kumchonga mfalme Daudi kutoka kwenye jiwe lilelile Mwaka 1501 na…

…akakabidhi kazi yake Mwaka 1504 na leo ni sanamu maarufu sana inayovutia watalii mamilioni kila mwaka.

Siku moja alipoulizwa na papa alifanikiwaje alisema…

…“Nilimuona Daudi ndani ya jiwe tayari, nilichofanya ni kuondoa kila kitu ambacho haikukuwa Daudi ili Daudi abakie na aonekane vizuri”

Kuna watu wengi sana ambao kwa nje wanaonekana si Kitu ila kumbe ndani wana Kitu kikubwa kimejificha.

Mara nyingine hata wewe Inawezekana wengine wakikuangalia wanaona jiwe tu ila kumbe ndani kuna “Daudi” – Kuna uwezo mkubwa umejificha, kuna Kipaji kikubwa ndani yako n.k

Unachotakiwa kufanya wiki hii ni kuanza kushughulikia kila tabia, udhaifu na visingizio ambavyo vinafanya Kitu kikubwa kilichopo ndani yako kisionekane.

Usikubali watu kama “Antonio” na “Augustino “ wakufanye ujione hauna thamani katika maisha yako.

Tambua kuwa wewe ni mgodi unaotembea, kuna Kiongozi mkubwa amejificha ndani yako…

…kuna bilionea ndani yako, kuna mfanyabishara mkubwa ndani yako, kuna mkurugenzi ndani yako n.k.

Uwe makini na “Maaugustino” na “Maantonio” utakakutana nao wakikuambia – Haufai, hauwezi, wewe si Kitu n.k – USIWAAMINI!!

Umeshawahi kukutana na akina “Augustino” na “Antonio” kwenye maisha yako?

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment