Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mahakama nchini Thailand imemuondoa madarakani Waziri Mkuu nchini humo Paetongtarn Shinawatra kwa sababu ya simu iliyovuja na aliyekuwa kiongozi wa Cambodia Hun Sen.
Waziri huyo alimpigia simu Hun Sen na kumuita “mjomba” kisha akazungumza vibaya kuhusu kamanda wa jeshi la Thailand.
Wakosoaji walimshtumu kwa kudhoofisha jeshi lenye nguvu la Thailand.
Paetongtarn aliomba msamaha baada ya kuvuja kwa simu hiyo, akidai ilikuwa “mbinu ya mazungumzo” huku kukiwa na mvutano mbaya wa mpaka na Cambodia.
Lakini Mahakama ya Kikatiba ya Thailand leo imetoa uamuzi kwamba “vitendo vyake vilikinzana na fahari ya taifa na kuzingatia maslahi ya kibinafsi zaidi ya nchi, ambayo ilikiuka kabisa au kushindwa kufuata viwango vya maadili vilivyowekwa”
Katika maoni yake ya kwanza baada ya uamuzi huo, Paetongtarn alikiri uamuzi huo, lakini akasema kwamba umesababisha “mabadiliko mengine ya ghafla” nchini Thailand, ambapo anakuwa kiongozi wa tano tangu 2008 kuondolewa madarakani na mahakama.
Naibu Waziri Mkuu wa Thailand sasa atachukua nafasi ya Paetongtarn kabla ya kura mpya kufanyika kumchagua waziri mkuu mpya.
DR Congo kususia mkutano wa amani wa Thabo Mbeki utakaofanyika Afrika Kusini

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imesema kuwa itasusia mkutano wa amani uliopangwa kufanyika mnamo mwezi Septemba nchini Afrika Kusini.
Mkutano huo ulioandaliwa na aliyekuwa Rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki umewaalika viongozi wa pande zote kwenye mzozo wa DR Congo, pamoja na kundi la waasi la M23 lenye kuungwa mkono na Rwanda.
Patrick Muyaya, msemaji wa serikali ya DRC amesema mkutano huo unaoongozwa na wakfu wa Mbeki haujapangwa kwa muda sahihi na hawajapendezwa nao.
“Tayari tuna njia tatu za kuongoza DRC kufikia amani,” alisema Muyaya wakati akidai kwamba taarifa kadhaa za awali za Thabo Mbeki zilionyesha aina ya kutojali ya hali ya sasa ya usalama mashariki ya Congo.
Alisema kuwa DRC inazingatia zaidi mchakato wa amani wa Washington na Doha na vile vile juhudi za pamoja za madhehebu mengi ya kidini huko Congo.
Wajumbe wa serikali na baraza la mawaziri la Rais Félix Tshisekedi walikuwa wamealikwa katika mkutano huo nchini Afrika Kusini.
Bado haijulikani wazi ikiwa M23 itashiriki katika mkutano huo, lakini kiongozi wa harakati za AFC/ M23, Corneille Nangaa alikuwa amealikwa.
Wakfu huo pia ulimwalika Rais wa zamani wa DR Congo, Joseph Kabila na viongozi wengine wakuu wa kisiasa na kibiashara ikiwa ni pamoja na Moïse Katumbi, Vital Kamerhe, Delly Sesanga, Martin Fayulu, Claudel Lubaya, Seth Kikuni na Jean- Jacques Lumumba.
Mkutano huo umepangwa kufanyika kati ya 3 na 6 Septemba.
Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zafikia hatua ya kuiwekea tena vikwazo vya Umoja wa Mataifa Iran

Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimeanza mchakato wa kurejesha vikwazo vikubwa vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran, vilivyoondolewa chini ya makubaliano ya 2015, huku mvutano ukiongezeka tena kuhusu mpango wa nyuklia wa Tehran.
Hatua hiyo itaanzisha kinachojulikana kama utaratibu wa ‘snapback’, ambao unaweza kusababisha kurejeshwa kwa vikwazo ndani ya siku 30.
Katika barua yake kwa Mkuu wa Sera wa Umoja wa Ulaya, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alisema nchi hizo tatu “hazina mamlaka ya kisheria” kuhuisha vikwazo hivyo na kwamba Urusi na China zote zinaunga mkono msimamo wa Iran.
Waziri huyo aliandika kwamba Iran iko tayari kuanza tena mazungumzo “ya haki na yenye usawa” kuhusu mpango huo unaobishaniwa iwapo pande nyingine zitaonesha “uzito na nia njema”.
Waziri wa fedha wa Israel atoa wito kunyakua maneo ya Gaza ikiwa Hamas haitasalimisha silaha

Waziri wa Fedha wa Israel Bezalel Smotrich ametoa wito kwa serikali siku ya Alhamisi kuanza kunyakua maeneo ya Ukanda wa Gaza ikiwa Hamas itaendelea kukataa kusalimisha silaha.
Wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Jerusalem, waziri wa siasa kali za mrengo wa kulia, ambaye anapinga vikali makubaliano yoyote na Hamas kumaliza vita vilivyodumu takriban miaka miwili katika Ukanda wa Gaza, aliwasilisha mpango wake wa “ushindi huko Gaza ifikapo mwisho wa mwaka.”
Chini ya pendekezo la Smotrich, Hamas itapewa uamuzi wa mwisho wa kusalimisha silaha zake na kuwaachilia mateka ambao bado wanashikiliwa huko Gaza tangu shambulio la vuguvugu la Oktoba 2023.
Smotrich pia alisema kwamba kama Hamas itakataa, Israel inapaswa kutwaa sehemu ya Ukanda wa Gaza kila wiki kwa muda wa wiki nne, na kuweka sehemu kubwa ya Ukanda wa Gaza chini ya udhibiti kamili wa Israel.
Alitoa wito kwa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu “kupitisha mpango huu kikamilifu na mara moja.”
Waziri wa fedha wa Israel atoa wito kunyakua maneo ya Gaza ikiwa Hamas haitasalimisha silaha

Waziri wa Fedha wa Israel Bezalel Smotrich ametoa wito kwa serikali siku ya Alhamisi kuanza kunyakua maeneo ya Ukanda wa Gaza ikiwa Hamas itaendelea kukataa kusalimisha silaha.
Wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Jerusalem, waziri wa siasa kali za mrengo wa kulia, ambaye anapinga vikali makubaliano yoyote na Hamas kumaliza vita vilivyodumu takriban miaka miwili katika Ukanda wa Gaza, aliwasilisha mpango wake wa “ushindi huko Gaza ifikapo mwisho wa mwaka.”
Chini ya pendekezo la Smotrich, Hamas itapewa uamuzi wa mwisho wa kusalimisha silaha zake na kuwaachilia mateka ambao bado wanashikiliwa huko Gaza tangu shambulio la vuguvugu la Oktoba 2023.
Smotrich pia alisema kwamba kama Hamas itakataa, Israel inapaswa kutwaa sehemu ya Ukanda wa Gaza kila wiki kwa muda wa wiki nne, na kuweka sehemu kubwa ya Ukanda wa Gaza chini ya udhibiti kamili wa Israel.
Alitoa wito kwa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu “kupitisha mpango huu kikamilifu na mara moja.”
Urusi yashambulia Makao makuu ya EU na kuua 23

Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen, ameeleza hasira yake kufuatia shambulio kubwa zaidi la Urusi mjini Kyiv tangu Julai, ambapo watu 23 akiwemo watoto wanne waliuawa na ofisi ya ujumbe wa EU pamoja na majengo jirani kuharibiwa.
Maafisa wa Ukraine wamesema makombora ya Urusi yaliharibu jengo la ghorofa tano katika wilaya ya Darnytskyi, na wengi wa waliokufa walikuwa humo.
Wengine kadhaa walijeruhiwa, wakiwemo watoto. Von der Leyen alisema makombora mawili yalipiga karibu na ujumbe wa EU umbali wa mita 50 pekee ndani ya sekunde 20, jambo alilolaani vikali.
Ofisi ya Baraza la Uingereza pia iliharibiwa. Jeshi la Ukraine liliripoti kuwa Urusi ilitumia karibu ndege zisizo na rubani 600 na zaidi ya makombora 30 ya masafa marefu katika shambulio hilo, likiwa kubwa zaidi mwezi huu.
Shambulio hilo lilitokea majira ya saa 9 alfajiri, likisababisha jengo la makazi kuporomoka. Vikosi vya uokoaji vilionekana wakiondoa kifusi na kutafuta manusura. Maafisa wamesema watoto waliouawa walikuwa na umri wa miaka 2, 14 na 17.
Kundi la kwanza la wahamiaji lawasili Rwanda kutoka Marekani

Kundi la kwanza la wahamiaji saba waliorejeshwa kutoka Marekani limewasili Rwanda katikati ya Agosti, kati ya jumla ya 250 wanaotarajiwa kupokelewa chini ya makubaliano na utawala wa Rais Donald Trump.
Serikali ya Rwanda imesema wanne wataendelea kukaa nchini humo, huku watatu wakichagua kurejea makwao.
Mashirika ya haki za binadamu yameonya kuwa mpango huu unaweza kukiuka sheria za kimataifa endapo wahamiaji watarudishwa katika nchi ambako wanaweza kukumbwa na mateso au ukiukwaji wa haki. Hata hivyo, msemaji wa serikali Yolande Makolo amesema wahamiaji wote watapatiwa msaada na ulinzi unaohitajika na serikali ya Rwanda.
Wahamiaji hao wanahifadhiwa na shirika la kimataifa na wanatembelewa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) pamoja na huduma za kijamii za Rwanda.
IOM imethibitisha kuwa imewapokea ili kutathmini mahitaji yao ya msingi. Serikali ya Rwanda inasema inaendelea na makubaliano haya kwa kuwa karibu kila familia nchini humo imewahi kupitia machungu ya ukimbizi kufuatia historia ya mauaji ya kimbari ya miaka ya 1990.
Rwanda pia imewahi kupokea karibu wakimbizi 3,000 kutoka Libya kati ya mwaka 2019 na 2025 kupitia mpango wa UNHCR na Umoja wa Afrika. Rwanda ilikuwa na makubaliano kama hayo na Uingereza mwaka 2022, lakini mpango huo ulifutwa na serikali ya Labour mwaka 2024 licha ya kulipwa pauni milioni 240 na kujengewa makazi ya wakimbizi.
Haijulikani iwapo makubaliano ya sasa na Marekani yanahusisha malipo ya kifedha. Aidha, Rwanda imekuwa sehemu ya mazungumzo ya amani yanayosimamiwa Washington kuhusiana na mzozo wa muda mrefu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, japokuwa Kigali inakanusha kuhusika na kundi la waasi wa M23 linalopigana nchini humo.
Liverpool, City ‘kutoboa’ Ligi ya Mabingwa Ulaya?

Vilabu vya Ligi Kuu ya Uingereza, Liverpool na Manchester City, vitakabiliana na miamba ya soka ya Ulaya, Real Madrid, katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa, huku Tottenham na Newcastle zote zikipangwa na mabingwa watetezi, Paris St-Germain.
Mfumo wa ligi unaoshirikisha timu 36 ulioanza msimu uliopita, utashuhudia timu sita za Ligi kuu England zikishiriki kwa mara ya kwanza, lakini hazitaweza kukutana hadi hatua ya mtoano.
Mbali na kukabiliana na Real Madrid, ambao wamewahi kuchukua kombe hili mara 15, Liverpool pia watakutana na Atletico Madrid na Inter Milan katika mechi zao nane. Timu ya Pep Guardiola, Manchester City, itakutana na Napoli na Borussia Dortmund.
Chelsea watacheza na miamba Barcelona na Bayern Munich, huku Arsenal wakicheza na Harry Kane wa Bayern na Inter.
Newcastle watarejea katika michuano hii kwa safari ya St James’ Park kuikabili Barcelona, huku Tottenham ambao walifuzu kwa kushinda Ligi ya Europa wakicheza na Dortmund na Monaco.
Mechi za kwanza zitachezwa Jumanne, Septemba 16, na raundi ya mwisho ya mechi za ligi itafanyika Januari 28, 2026.
Orodha ya mechi za Ligi Kuu ya Uingereza:
Liverpool: Real Madrid (nyumbani), Inter Milan (ugenini), Atletico Madrid (nyumbani), Eintracht Frankfurt (ugenini), PSV Eindhoven (nyumbani), Marseille (ugenini), Qarabag (nyumbani) na Galatasaray (ugenini).
Manchester City: Borussia Dortmund (nyumbani), Real Madrid (ugenini), Bayer Leverkusen (nyumbani), Villarreal (ugenini), Napoli (nyumbani), Bodo/Glimt (ugenini), Galatasaray (nyumbani) na Monaco (ugenini).
Chelsea: Barcelona (nyumbani), Bayern Munich (ugenini), Benfica (nyumbani), Atalanta (ugenini), Ajax (nyumbani), Napoli (ugenini), Pafos (nyumbani) na Qarabag (ugenini).
Arsenal: Bayern Munich (nyumbani), Inter Milan (ugenini), Atletico Madrid (ugenini), Club Brugge (nyumbani), Olympiacos (ugenini), Slavia Prague (nyumbani), Kairat Almaty (ugenini) na Athletic Bilbao (nyumbani).
Tottenham: Borussia Dortmund (nyumbani), Paris St-Germain (ugenini), Villarreal (nyumbani), Eintracht Frankfurt (ugenini), Slavia Prague (nyumbani), Bodo/Glimt (ugenini), Copenhagen (nyumbani) na Monaco (ugenini).
Newcastle: Barcelona (nyumbani), Paris St-Germain (ugenini), Benfica (nyumbani), Bayer Leverkusen (ugenini), PSV (nyumbani), Marseille (ugenini), Athletic Bilbao (nyumbani) na Union SG (ugenini).
Liverpool, Arsenal, Manchester City, Chelsea na Newcastle zilipata nafasi zao kwa kumaliza ndani ya tano bora ya Premier League. Tottenham ilipata nafasi yake kwa kushinda Ligi ya Europa.
Timu iliyoshika nafasi ya sita, Aston Villa, ilibidi iridhike na Ligi ya Europa, pamoja na Nottingham Forest.
Washindi wa Kombe la FA, Crystal Palace, wako kwenye Ligi ya Conference, baada ya kushushwa kutoka Ligi ya Europa kutokana na sheria za umiliki wa vilabu vingi.
Mechi ya fainali ya ligi ya mabingwa msimu huu itapigwa May 30, 2026 huko Budapest, Hungary.
Jose Mourinho ‘atimuliwa’ Fenerbahce

Fenerbahce imeachana na Jose Mourinho ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kujiunga na timu hiyo. Kuondoka kwa mreno huyo kumekuja siku mbili baada ya klabu hiyo ya Uturuki kuondolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa na timu ya Benfica.
Taarifa ya klabu hiyo ilisema Mourinho “aliachana” na klabu hiyo, na kumshukuru mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 62 kwa juhudi zake.
“Tunamtakia mafanikio katika kazi yake ya baadaye,” iliongeza taarifa hiyo.
Mourinho, ambaye amekuwa kocha wa vilabu 10 ikiwemo Chelsea, Manchester United na Tottenham, aliiongoza Fenerbahce kushika nafasi ya pili kwenye ligi kuu nchini Uturuki wakati wa msimu wake wa kwanza, lakini alikumbana na mizozo kadhaa.
Mabingwa Galatasaray walisema watamchuklia hatua za kisheria Mourinho, baada ya kumtuhumu kwa “kauli za kibaguzi” kwenye mchezo wa sare ya 0-0 wa mwezi Februari.
Mourinho alikanusha madai hayo, akisema yeye ni “sio mbaguzi, na akaifungulia kesi klabu hiyo akitaka kulipwa fidia ya £41,000.
Mourinho amekuwa mkosoaji wa mara kwa mara wa waamuzi nchini Uturuki, kwa sababu hiyo alipewa adhabu ya kufungiwa michezo minne, baadaye ikapunguzwa hadi miwili kutokana na maneno yake kuhusu waamuzi.
Alitoa maneno ya kutuhumu waamuzi baada ya mechi baina ya Fenerbahce dhidi ya Galatasaray msimu uliopita.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.