Urusi yashambulia Makao makuu ya EU na kuua 23

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen, ameeleza hasira yake kufuatia shambulio kubwa zaidi la Urusi mjini Kyiv tangu Julai, ambapo watu 23 akiwemo watoto wanne waliuawa na ofisi ya ujumbe wa EU pamoja na majengo jirani kuharibiwa.

Maafisa wa Ukraine wamesema makombora ya Urusi yaliharibu jengo la ghorofa tano katika wilaya ya Darnytskyi, na wengi wa waliokufa walikuwa humo.

Wengine kadhaa walijeruhiwa, wakiwemo watoto. Von der Leyen alisema makombora mawili yalipiga karibu na ujumbe wa EU umbali wa mita 50 pekee ndani ya sekunde 20, jambo alilolaani vikali.

Ofisi ya Baraza la Uingereza pia iliharibiwa. Jeshi la Ukraine liliripoti kuwa Urusi ilitumia karibu ndege zisizo na rubani 600 na zaidi ya makombora 30 ya masafa marefu katika shambulio hilo, likiwa kubwa zaidi mwezi huu.

Shambulio hilo lilitokea majira ya saa 9 alfajiri, likisababisha jengo la makazi kuporomoka. Vikosi vya uokoaji vilionekana wakiondoa kifusi na kutafuta manusura. Maafisa wamesema watoto waliouawa walikuwa na umri wa miaka 2, 14 na 17.

Kundi la kwanza la wahamiaji lawasili Rwanda kutoka Marekani

Msemaji wa serikali Yolande Makolo anasema wale wanaoamua kusalia Rwanda watapata "msaada na ulinzi ufaao"

Kundi la kwanza la wahamiaji saba waliorejeshwa kutoka Marekani limewasili Rwanda katikati ya Agosti, kati ya jumla ya 250 wanaotarajiwa kupokelewa chini ya makubaliano na utawala wa Rais Donald Trump.

Serikali ya Rwanda imesema wanne wataendelea kukaa nchini humo, huku watatu wakichagua kurejea makwao.

Mashirika ya haki za binadamu yameonya kuwa mpango huu unaweza kukiuka sheria za kimataifa endapo wahamiaji watarudishwa katika nchi ambako wanaweza kukumbwa na mateso au ukiukwaji wa haki. Hata hivyo, msemaji wa serikali Yolande Makolo amesema wahamiaji wote watapatiwa msaada na ulinzi unaohitajika na serikali ya Rwanda.

Wahamiaji hao wanahifadhiwa na shirika la kimataifa na wanatembelewa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) pamoja na huduma za kijamii za Rwanda.

IOM imethibitisha kuwa imewapokea ili kutathmini mahitaji yao ya msingi. Serikali ya Rwanda inasema inaendelea na makubaliano haya kwa kuwa karibu kila familia nchini humo imewahi kupitia machungu ya ukimbizi kufuatia historia ya mauaji ya kimbari ya miaka ya 1990.

Rwanda pia imewahi kupokea karibu wakimbizi 3,000 kutoka Libya kati ya mwaka 2019 na 2025 kupitia mpango wa UNHCR na Umoja wa Afrika. Rwanda ilikuwa na makubaliano kama hayo na Uingereza mwaka 2022, lakini mpango huo ulifutwa na serikali ya Labour mwaka 2024 licha ya kulipwa pauni milioni 240 na kujengewa makazi ya wakimbizi.

Haijulikani iwapo makubaliano ya sasa na Marekani yanahusisha malipo ya kifedha. Aidha, Rwanda imekuwa sehemu ya mazungumzo ya amani yanayosimamiwa Washington kuhusiana na mzozo wa muda mrefu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, japokuwa Kigali inakanusha kuhusika na kundi la waasi wa M23 linalopigana nchini humo.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment