Unapoamka unavutia asubui unavutia vitu vipi maishani.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mara tu unapoamka akili yako itaanza kuvutiwa na vitu ambavyo ni HASI zaidi kuliko vile ambavyo ni CHANYA…

Hii ni kwa sababu mawazo yako kwa asilimia kubwa ni hasi.

Kulingana na utafiti wa Taasisi ya Akili nchini marekani ilionesha kuwa takribani 80% ya mawazo tunayowaza kila siku huwa ni Hasi.

Hii ndio maana ni rahisi sana mtu ukaamka na kuanza kulalamika mambo ambavyo hayaendi sawa.

Ukaanza kulaumu jinsi ambavyo umekosa kazi uliyoitarajia.

Jinsi ulivyopata hasara na kupoteza PESA.

Jinsi ambavyo UMEUMIZWA HISIA zako n.k

Haya yote yanaendelea kudhoofisha FURAHA yako na kukuletea MSONGO wa MAWAZO kila siku.

Ili kuwa wa tofauti ni lazima uamue kuulinda MOYO na AKILI yako isipatwe na shambulizi hili.

Njia nzuri sana ya kufanya hivyo ni kupitia “Practice of Gratitude”(Kujizoeza Kushukuru).

Mara nyingi watu wengi hawaoni sababu ya KUSHUKURU kama wanavyoona kwa haraka sababu za KULAUMU.

Kumbuka kuna mengi sana ambayo unaweza kushukuru leo kabla haujaanza kulaumu.

Kabla haujasema HAUNA KAZI kumbuka kushukuru kwamba BADO UNAPUMUA.

Kabla haujasema UMEUMIZWA kumbuka kuna wengine waliuwawa kwenye mahusiano.

Kabla haujamlaumu Mungu kwa ugonjwa wako kumbuka kuna watu wako ICU mwaka wa tatu sasa HAWAJAWAHI KUONGEA.

Kabla haujalaumu mwenzi wako kumbuka MEMA aliyowahi kukufanyia.

Kabla haujaanza siku kwa kulalamika hauna PESA kumbuka ambao jana wamelala na NJAA na leo hawajui WATAKULA nini n.k

Kwa nini usianze siku yako kwa KUJILAZIMISHA KUSHUKURU?

Kumbuka ulichonacho unachokiona KIDOGO na KUKIDHARAU kuna watu WANAKESHA na WANAOMBA WAKIPATE.

Kabla haujalaumu, kulalamika au kusema mambo HASI, anza siku yako kwa Kushukuru.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment