Giza linatanda tumaini,inapotea.

Kuna wakati akili inachoka mwanga unapotea giza linatanda tumaini linaisha kabisa hofu inaingia kwasababu matatizo yaliyokuzunguka ambayo huoni kama unatoka

○Katika maombi Mungu amenisemesha jambo hili nikutie moyo dada angu najua umefika mahali akili yako haina matunda tena

○Ninajua mama ndoa yako haina amani na unatamani kama tu ungetoka kwenye hiyo ndoa maana mume wako amebadilika sana moyo umejaa huzuni tu maana hukutegemea

○Ninajua Baba maisha yamekuwa magumu kwako kazi hamna uchumi umeyumba kila unachojaribu hakikupi mwanga na matokeo uliyoyategemea akili na mwili wako vimechoka kabisa

○Mungu amenitumia niseme na wewe wala ujumbe huu haujaja kwako kwa Bahati mbaya hata kama huoni mwanga endelea tu kuamini hakuna usiku usiokuwa na asubuhi

Zaburi 27:7:9

Ee BWANA, usikie, kwa sauti yangu ninalia,Unifadhili, unijibu.
Uliposema, Nitafuteni uso wangu,Moyo wangu umekuambia,BWANA, uso wako nitautafuta.
Usinifiche uso wako,Usijiepushe na mtumishi wako kwa hasira.Umekuwa msaada wangu, usinitupe,Wala usiniache, Ee Mungu wa wokovu wangu.

○Ninakuombea mpendwa wangu Mungu ninaemtumikia akasikie sauti ya kilio chako akakujibu upesi

○Wala hatakuacha na kukufisha uso wake Yeye ni msaada wako atakujibu endelea kumwamini na kumtumainia

○Kama vile usiku ulivyo na asubuhi nami ninaamlu pambazuko litokee sasa kwenye maisha yako katika jina la Yesu

○Mpendwa wangu kila lenye mwanzo huwa lina mwisho pia nami ninakuombea mwisho wa matatizo yako unatokea sasa na nyakati mpya zikaachiliwe kwako katika jina la Yesu

●Kama unaamini comment ” Bwana komesha mateso kwenye maisha yangu na achilia nyakati mpya kwangu” na itakuwa katika jina la Yesu


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment