Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Ukiamua kutotumia UWEZO WAKO MKUBWA(Your Hidden Potential) watu hawatakuwa na tatizo na wewe.Hakuna mtu atakuwa adui yako,hakuna mtu atapigana kukushusha,hakuna mtu atakuchafua:Ukawaida unafanya kila mtu awe “comfortable” na wewe.Ukiwa kawaida,wewe si TISHIO kwa sababu unafanana na kila mtu.
.
Shida ni pale unapoamua kuwa wa TOFAUTI,unapokata Shauri kuwa utaanza kuishi maisha tofauti na wengine.Pale unapotaka kutoka katika mfumo ambao kila mtu ameuzoea.Wanadamu wanapenda kifo cha wengi na wanakiita Harusi,ukianza kuonyesha hautaki kuwa nao unageuka adui yao.
.
Ukianza kusema ama kufanya mambo ya tofauti hapo ndipo utaanza kukaribisha watu wanaokupinga,watu watakaokuambia hauwezi na watu watakaoanza kuwa maadui zako kwa sababu zisizojulikana.
.
Unapoamua kuanza kuishi ndoto yako,kuanza kutumia uwezo wako,kutoka katika mfumo wa MAISHA ambao umezoeleka:Jiandae kisaikolojia KUPINGWA,KUKATALIWA na KUPIGWA ZENGWE.
.
Usishangae watu ambao walikuwa hawana tatizo na wewe Siku zote,Ukianza tu KUONYESHA UWEZO WAKO wanaanza kuwa maadui na kukushusha.Ndio MAISHA yalivyo.
.
KUWA TOFAUTI KUNA GHARAMA ILA KUNA FAIDA KUBWA.Uko tayari kuwa Tofauti?
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.