Let them ridicule you, laugh at you, hurt you & ignore you but never let them stop you.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Apoorve Dubey aliwahi kusema “Waache WAKUDHIHAKI,WAKUCHEKE,wakuumize,wakupuuze ila USIWARUHUSU WAKUZUIE(Let them ridicule you, laugh at you, hurt you & ignore you but never let them stop you).

.

Kuna hatua kwenye maisha yako utaipitia na moja kati ya haya au yote haya yatakutokea.Watu wanafanya haya kwa sababu mbalimbali:

.

1)Kuna ambao HAWAAMINI katika maono yako.Wanaona kama vile UNA NIA makuu kuliko uwezo wako.Wangepata nafasi ya kukushauri basi wangekuambia UACHANE kabisa na maono uliyonayo.Watu hawa kwa namna nyingine wanaona kama UNACHOTAKA kufanya HAUNA UWEZO NACHO.

.

2)Kuna ambao wanaona UNAFANYA HARAKA sana.Wengi wao kwa sababu WALITUMIA Muda mrefu kupata matokeo fulani ama wana mifano ya watu ambao walichukua muda mrefu-Wanaamini kuwa na wewe inatakiwa uchukue MUDA mrefu pia:Hawaamini kama UNAWEZA kupata matokeo ndani ya muda mfupi kuliko WALIVYOZOEA.

.

3)Kuna ambao watafanya haya ili tu UACHE kwa sababu kwa kufanikiwa kwako “unawaprove wrong”.Kuna wengi ambao WALIWAAMBIA watu na Walisema kwa kujiamini kuwa HAUTAWEZA.Wanapoona unaanza KUFANIKIWA watafanya kila njia ili USISOGEE ili ionekane walichosema kilikuwa ni KWELI.

.

Kwa vyovyote vile amua jambo moja:Bila kujali MANENO yao ama MATENDO yao-HAUTASIMAMA bali UTASONGA MBELE.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment