Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kuna HISIA ambayo HAUWEZI KUIKWEPA kwenye MAISHA yako kama unataka kuwa mshindi.
Kila unayemuona MSHINDI Leo alipata hizo hisia…
Kila MWANAJESHI aliwahi kuipata…
Kila RAIS amewahi kuipitia…
Kila MFANYABIASHARA amewahi kuipitia…
…ni ile hali ya KUTAKA KUISHIA NJIANI.
Haya ni maneno niliyowahi kuyasikia kutoka kwa muhubiri na mwandishi nguli duniani, T.D Jakes…
…aliiita “The Urge To Give Up”.
Usifikiri wewe pekee au wewe ndio wa kwanza kupitia hali hii.
Unaona Kama Biashara imefika mwisho huwezi Kuinuka.
Mahusiano yamefika mwisho hakuna namna unaweza Kuyaokoa.
Ndoto yako imefika mwisho n.k.
Kitakachotofautisha ni UTAFANYA nini BAADA YA LEO.
Ukiamua KUACHA au KUKATA TAMAA ujue utakuwa umefunga MLANGO mkubwa ambao ulikuwa unakaribia KUFUNGUKA.
Ni kweli unasikia MAUMIVU MAKALI ila USIKATE TAMAA.
Washindi ni wale ambao wanapopitia hali Kama unayopitia Leo WANAJILAZIMISHA kuchukua HATUA MOJA ZAIDI.
Leo, UNAWEZA KUBADILISHA HALI YAKO KAMA UTAAMUA KUWA HAUTAKATA TAMAA.
Kujifunza zaidi nashauri usome eBook ya “Jinsi Ya Kufanikiwa Katikati Ya Nyakati Ngumu”
(Pia ipo Version yake ya kiingereza inaitwa “Surviving The Crisis”, Utachagua unataka cha kiswahili ya cha kiingereza)
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.