Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kila mwaka ni Muhimu,kila Mwezi ni Muhimu,Kila Siku ni Muhimu,Kila saa ni Muhimu,kila dakika ni muhimu,kila sekunde ni Muhimu.
Siku zote usisahau kuwa tofauti ya watu wanaoitwa ordinary(wa kawaida) na wale ambao wanazidi kawaida(extra-ordinary) ni Ile EXTRA.Muda ambao unaweza kuleta tofauti kwenye maisha yako ni Ile ambao unaonekana uko kwenye MAMLAKA yako kwa 100%.
Ukigundua kuwa wewe ni mtu ambaye ukiwa na muda wako mwenyewe basi huwa unautumia kwa kulala tuu,kupiga story tuu n.k na hakuna kitu chochote cha kujenga kuelekea unakotaka kwenda basi ujue umekosa NIDHAMU YA MAISHA.
Kama wewe ni muajiriwa na Siku zote za wiki umeuza muda wako kwa mwajiri wako na unajenga ufalme wake-Siku ambazo huendi huko ndio unatakiwa kuzitumia kujenga ufalme wako pia.Bila KUJALI ni HATUA ndogo kiasi gani,JARIBU KUFANYA KITU kinachochangia kwenye HATIMA YAKO LEO.
Leo amua kuwa na ratiba ya tofauti kuliko jumamosi zote ulizozoea.Usikubali ipite bila kufanya kitu cha KUCHANGIA kwenye HATUA ZAKO ZA KWENDA MBELE.Usiishie kuangalia mpira tu,usiishie kuangalia movie tu,usiishie kulala tu,usiishie kuzurua tu,usiishie kuchart tu,FANYA KITU UTAKACHOJIVUNIA MIAKA 10 IJAYO LEO.
KILA SIKU NI MUHIMU.FANYA KITU EXTRA LEO!
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.