Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Al-Ittihad wanataka kumsajili Bruno Fernandes wa Manchester United na tayari wamefanya mazungumzo na wawakilishi wa kiungo huyo wa kati wa Ureno mwenye umri wa miaka 30. (Sun)
Tottenham wako tayari kupiku majaribio ya Crystal Palace kumsajili kiungo wa Morocco Bilal El Khannouss kutoka Leicester baada ya kumkosa mshambuliaji wa Uingereza Eberechi Eze, 27. (Africa Foot)
Napoli wanaweza kukamilisha dili la kumnunua mshambuliaji wa Manchester United na Denmark Rasmus Hojlund, 22, ifikapo Jumatatu huku wakitafuta mbadala wa haraka wa mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 32. (Corriere Dello Sport)

Atalanta iko tayari kuchuana na West Ham na Nottingham Forest katika mbio za kumsajili kiungo wa kati wa Monaco na Ufaransa Soungoutou Magassa. (Footmercato )
West Ham wanavutiwa na kiungo wa kati wa Italia Lorenzo Pellegrini, 29, ambaye amevuliwa unahodha wa Roma. (Sky Sport Italia)
Borussia Dortmund wanakaribia kusajili wachezaji wawili wa Chelsea, huku mshambuliaji Muingereza Carney Chukwuemeka, 21, akiwa amekubali uhamisho wa kudumu katika mkataba wa thamani ya euro 25m (£21.7m) huku beki wa Argentina mwenye umri wa miaka 20 Aaron Anselmino akihamia kwa mkopo. (Sky Sport Germany)

Roma wanataka kumsajili beki wa pembeni wa Ugiriki Kostas Tsimikas, 29, kwa mkopo kutoka Liverpool. (Giancluca di Marzo)
Real Betis bado wanashughulikia mpango wa kumsajili winga wa Manchester United mwenye umri wa miaka 25 kutoka Brazil Antony. (Fabrizio Romano)
Brentford wanafikiria kumnunua mlinzi wa Coventry Muingereza Bobby Thomas, 24, kama watamuuza mlinzi wa Jamhuri ya Ireland Nathan Collins, pia 24, kabla ya tarehe ya mwisho ya uhamisho. (Football Insider)

Como wamekataa dau lililoboreshwa la Tottenham la euro 45m (£39m) kumnunua kiungo wa kati wa Argentina Nico Paz, 20. (Nicolo Schira)
Klabu inayoshiriki ligi daraja la kwanza Derby imefikia makubaliano na Sturm Graz kumsajili beki wa kulia wa Scotland Max Johnston mwenye umri wa miaka 21. (Florian Plettenberg)
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.