Tanzania, Kenya zafungasha virago-michuano ya CHAN 2024:

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Taifa Stars walishindwa kutamba nyumbani dhidi ya Morocco

Timu za taifa za Kenya na Tanzania zimeaha mashindano ya CHAN hii leo baada ya kufungwa katika mechi za robo fainali.

Katika mechi ya awali iliyochezwa katika uga wa Kasrani jijini Nairobi

Kenya ilitolewa na Madagascar kupitia mikwaju ya penati baada ya kutoka sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.

Tanzania imepoteza mchezo ndani ya dakika 90 katika uwanja wa Benjamin Mkapa kwa kufungwa goli moja bila majibu.

Mashindano ya mwaka huu ya CHAN yanaandaliwa na nchi tatu jirani za Afrika Mashariki, Kenya, Uganda na Tanzania.

Sasa matumaini yote ya wenyeji yanaelekezwa Uganda ambao wanashuka dimbani kesho dhidi ya Senegal.

Kenya yatawala mchezo

h

Kenya walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Alphonse Omoja dakika ya 38, kabla ya Razafimahatratra wa Madagascar kusawazisha dakika ya 60.

Baada ya kutoka ya sare ya 1-1 katika dakika 120, Madagascar walishinda 4-3 kwa mikwaju ya penalti, huku Toky Rakotondraibe akifunga mkwaju wa penalti baada ya Alphonce Omija kukosa.

Harambee Stars, ilikuwa ikiwania kutinga nusu fainali ya kwanza ya bara baada ya miaka 38.

Tanzania yashindwa kuendeleza ubabe

Tanzania kama ilivyokuwa kwa Kenya ilitawala kipindi cha kwanza na kukosa nafasi kadhaa za wazi za kufunga magoli.

Katika dakika ya 65 ya kipindi cha pili Morocco ilizima ndoto za Tanzania kwa holi safi lililofungwa na mshambuliaji Oussama Lamlaoui.

Tanzania ambayo iliongoza kundi B kwa kutinga robo fainali kibabe bila kufungwa hata mechi moja ikashindwa kendeleza ubabe mbele ya Morocco baada ya hapo.

Morocco imetwaa ubingwa wa CHAN mara mbili huku Taifa Stars ikitinga hatua hii kwa mara ya kwanza baada ya kushiriki mara tatu.

Awali Kocha wa Taifa Stars Hemed Suleiman alisema kuelekea mchezo huo “Nimeangalia makundi yote naamini kwamba kila timu katika kundi lolote ni mzuri na inaweza kuleta ushindani. Sisi tupo tayari kukabiliana na Morocco.”

Katika hatua ya makundi, Morocco ilikuwa tayari imeshinda mechi tatu na kuchapwa moja dhidi ya Kenya.

Imefunga mabao manane sawa na wastani wa kufunga mabao mawili katika kila mechi na kuruhusu mabao matatu.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment