Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Manchester City bado wanamtaka winga wa Brazil Rodrygo, mwenye umri wa miaka 24, ambaye Real Madrid wamemuwekea thamani ya takriban £69.3m (ESPN)
Hata hivyo, Arsenal pia wanamnyatia Rodrygo, huku Liverpool nao wakionesha nia kwa kuwa wanatafuta mbadala wa mshambuliaji wa Colombia Luis Diaz, 28, aliyehamia Bayern Munich mapema majira ya kiangazi haya. (Teamtalk)
Ange Postecoglou na Jose Mourinho ni miongoni mwa wanaoweza kupewa kazi ya kuinoa Nottingham Forest endapo Nuno Espirito Santo atafutwa kazi. (Sun)
Aston Villa wanaonekana kukosa fursa ya kumsajili mshambuliaji wa Senegal Nicolas Jackson, 24, kutokana na thamani ya Chelsea ya £70m kuwa kikwazo. (Sun).

Nicolas Jackson
Real Madrid wanamfuatilia kiungo wa Uingereza Adam Wharton, mwenye umri wa miaka 21, wa Crystal Palace. (AS – in Spanish)
Kipa wa kimataifa wa Cameroon Andre Onana, 29, anatarajiwa kubaki Manchester United, licha ya kuwepo kwa sintofahamu kuhusu mustakabali wake na uvumi kwamba klabu inaweza kuhamia kwa kipa wa Royal Antwerp, Senne Lammens, raia wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 23. (Mail)
Antwerp wanataka karibu £17m kwa Lammens, ambaye bado hajachezea timu ya taifa ya wakubwa ya Ubelgiji. (Sun)
Tottenham wako tayari kutoa ofa iliyoboreshwa ya zaidi ya £60m kwa ajili ya kumnasa winga wa Brazil Savinho, mwenye umri wa miaka 21, kutoka Manchester City. (Fabrizio Romano)

West Ham wamewasilisha ofa kwa Monaco kwa ajili ya Soungoutou Magassa, mwenye umri wa miaka 21, na wanajitahidi kukamilisha dili la kiungo huyo wa timu ya taifa ya vijana ya Ufaransa chini ya miaka 21. (Guardian)
Hata hivyo, Monaco wamekataa ofa ya awali yenye thamani ya takriban £14m pamoja na nyongeza ya £2.6m, ingawa wanatarajia West Ham watarudi na ofa mpya nzuri zaidi. (Footmercato)
Everton wamewasiliana na Villarreal kuhusu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Cameroon Etta Eyong, mwenye umri wa miaka 21. (El Chiringuito)
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.