Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Tony Robins aliwahi kusema “Ni wakati wa kufanya maamuzi ndio hatima yako inatengenezwa”(It’s the moment of decision when your destiny is shaped).Moja ya uwezo ambao unatakiwa kuujenga kwenye maisha yako ni kufanya maamuzi kuhusiana na mambo muhimu bila HOFU ya watu ama MATOKEO ya maamuzi yako.Kuna mambo kadhaa ya kuyafahamu:
.
1)Kuna aina ya maamuzi ambayo wewe peke yako ndio utaelewa umuhimu wake kwa wakati huo na kila anayekuzunguka hataelewa na hivyo hatakusapoti.Aina hii ya maamuzi wengine wataelewa na kukubaliana na wewe Muda mrefu ukishapita,Ukiwa na aina hii ya maamuzi usisubiri kila mtu akuelewe,chukua hatua leo na uwe tayari kusimama peke yako.
.
2)Kuna maamuzi ambayo unajua ni muhimu kwako kuyafanya ila Matokeo yake yatakuwa ni wewe kupitia aina fulani ya maumivu.Pengine yatakuletea maumivu ya kihisia,utapoteza watu,heshima,Fedha au utalazimika kuanza upya.Mara nyingi maamuzi haya huwa unajua UMUHIMU wake Ila hauyafanyi kwa kukwepa MAUMIVU.Kumbuka Kadiri unavyojichelewesha ndivyo maumivu yatakuja kuwa makali,ni bora Ufanye maamuzi leo.
.
3)Kuna maamuzi ambayo yamefichwa katika Muda,mafanikio ya maamuzi yako yatategemea uharaka wako wa kuamua leo,ukichelewa kuchukua hatua ukayafanya kesho utapishana na Fursa kubwa ambayo wakati mwingine haitajirudia kabisa katika maisha yako.Sio kila maamuzi ni ya kuyaghairisha,kuna mengine ukighairisha hupati tena fursa hiyo.Mara nyingi haya ni maamuzi ambayo yanatuweka Njia panda “Nifanye,nisifanye”.
.
Leo anza siku yako kwa kufanya maamuzi sahihi kuhusiana na jambo linalokukabili.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.