USIKUBALI KUUA NDOTO YAKO.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Watu ambao hawana ndoto kubwa.

Ndio, kuna watu wanaokuzunguka ambao wenyewe…

Hawana ndoto kubwa zaidi ya walivyo leo.

Yaani, kwa malengo waliyokuwa nayo kwenye maisha yao ni…

Kuwa wameshafika mwisho.

Wanapokuona unapambana, wanashangaa unapambania nini.

Kuna wengine, kile ulichonacho ndio ndoto yao kubwa.

Kwa vigezo vyao, wanaona umeshafika.

Hii ndio maana, ni muhimu sana kujizungushia na watu ambao…

Wana ndoto kubwa zaidi ili wakupe hamasa.

Ni hivi, ukubwa wa ndoto yako utachukua “size” ya…

Wastani wa ndoto zinazokuzunguka.

Usipokuwa makini utakuwa ni samaki mkubwa kwenye mto mdogo.

Kagua watu wanaokuzunguka…

Wanakupa HAMASA?

Au wanasababisha UNARIDHIKA na kujiona UMEFIKA?

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment