Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kwa mujibu wa utafiti uliowahi kufanywa na Benki ya Barclays na kuchapishwa mwaka 2014 mwezi May (Financial Well-Being: The Last Taboo in the Workplace?)…
…Ulionesha kuwa mtu huishi kwa amani ya moyo zaidi anapokuwa na akiba ya dharura ya kutosha (Emergency Fund) kuliko pale anapoongezewa mshahara (Pay Rise).
Hii humfanya mtu awe na utulivu wa kisaikolojia ya akili…
…na kumpa uwezo wa kutulia na kufanya maamuzi sahihi kila wakati.
Ushauri ni kuwa, kwenye kila pesa unayopata ni muhimu kuwa na kiasi fulani unachoweka akiba…
..kwa ajili ya changamoto kubwa za kifedha zisizotarajiwa (Financial Shock).
Sifa ya pesa hii ni pamoja na iwe ni Cash
(Sio kitu ambacho utataka kuuza na kikasumbua baadaye)…
…dhumuni kubwa sio kupata faida bali uweke sehemu ambayo ukiitaka wakati wowote utaipata.
Ushauri ni kuwa, inatakiwa ifikie kiwango sawa na jumla ya matumizi yako ya msingi ya miezi sita.
(Yaani kama matumizi yako ya lazima kwa mwezi ni 10,000/= AU 1,000,000 TZ basi akiba yako ya dharura wakati wote haitakiwi kuwa chini ya 6,000,000/=) AU 60,000 KSH
Jifanyie tathmini leo na angalia namna ya kuanza kutengeneza mfuko huu kwa faida yako mwenyewe.
Kama umechoka hali ya kifedha uliyonayo kwa kipindi kirefu.
Na, je unataka uendelee kutumia mbinu zile zile ulizotumia miaka yote na hazijakupa matokeo?
Au unataka nikupe maarifa yaliyowasaidia mamia ya watu kufikia malengo yao ya kifedha kwa kasi?
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.