Mazungumzo ya mkataba wa Plastiki yakwama

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Mazungumzo ya kimataifa ya kutafuta mkataba wa kihistoria wa kukomesha uchafuzi unaosababishwa na plastiki yamekwama.

Mazungumzo hayo ya Umoja wa Mataifa ya duru ya sita katika kipindi cha chini ya miaka mitatu, yalipaswa kukamilika siku ya Alhamisi lakini nchi ziliendelea kujadiliana hadi usiku wa manane kwa matumaini ya kupata suluhu.

Bado kuna mgawanyiko kati ya kundi la zaidi ya mataifa 100 linalotaka kuzuiliwa kwa uzalishaji wa plastiki huku mataifa yenye mafuta yakishinikiza kuzingatia uchakataji upya.

Wakizungumza mapema, wajumbe wa Cuba walisema kuwa nchi “zimekosa fursa ya kihistoria lakini inabidi tuendelee”.

Mazungumzo hayo yalianzishwa mnamo mwaka 2022 kama hatua iliyochukuliwa kutokana na ushahidi unaoongezeka wa kisayansi wa hatari za uchafuzi wa plastiki kwa afya ya binadamu na mazingira.

Licha ya manufaa ya plastiki kwa karibu kila sekta, wanasayansi wanawasiwasi sana juu ya kemikali zinazoweza kuwa na sumu, ambazo zinaweza kujitokeza kutokana na plastiki inapovunjika na kuwa vipande vidogo vidogo.

Plastiki ndogo ndogo zimegunduliwa katika udongo, mito, hewa na hata kwenye viungo katika mwili wa binadamu.

Nchi zilikuwa na makataa ya awali ya kupata mkataba juu ya suala hili kufikia mwishoni mwa Desemba mwaka jana, lakini zilishindwa kufikia makubaliano.

Graham Forbes, mkuu wa wajumbe wa shirika la Greenpeace kwenye mazungumzo ya Mkataba wa Kimataifa wa Plastiki, alisema: “Kutoweza kufikia makubaliano huko Geneva lazima iwe mwamko mpya ulimwenguni: kukomesha uchafuzi wa plastiki kunamaanisha kukabili masilahi ya mafuta ya kisukuku moja kwa moja.

Mwenyekiti alitangaza kuwa mazungumzo hayo yataanza tena siku nyingine.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment